Neno Goita ni jina linalotumika katika kuliita tatizo la
kuvimba kwa tezi ya thairoidi iliyo katika eneo la shingo. Kiufasaha, huu ni ugonjwa wa tezi ya
thairoidi. Ugonjwa huu pia unaweza
kutokea bila kuonekana uvimbe katika eneo hilo.
Ugonjwa huu unaonekana kuwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume, hasa
wale wanawake wasiopata muda wa kutosha wa kupumzika na kupata utulivu.
Dalili za Ugonjwa wa
Kuvimba Tezi ya Shingo (GOITER)
Dalili za mwanzoni za goita kwa kawaida huwa ni za muda
mfupi na hutokea kama mabadiliko madogo ya kihisia na huweza kupitia bila
kugundulika. Baadae mtiririko wa dalili
nyingine kama vile huzuni, kupoteza uwezo wa kuzingatia na kulia vinaweza
kuonekana vikiambata na kuharibika kwa hisia.
Pia mgonjwa mwenye tatizo hili huwa anakwazika kirahisi sana.
Kunaweza pia kukawa na kuvimba kwa tezi ya shingo lakini
hili haliashirii ukubwa wa tatizo kwani hata tatizo linapokuwa kubwa mara
nyingine inawezekana usionekane uvimbe ulio wazi. Dalili hizi huweza kufuatiwa na hisia za
uchovu uliopitiliza na kutetemeka kwa mikono pamoja na ukosefu wa nguvu za
kuwezesha kutumia misuli ya aina yoyote mwilini. Kwa baadhi ya wagonjwa macho huweza kutokeza
kwa nje.
Kupungua kwa uzito ni kati ya dalili zinazoweza kujitokeza zaidi kwa wale wanaoumwa ugonjwa huu na huweza kudumu mpaka kufikia hatua
ambapo mgonjwa anajisikia kuwa mdhaifu kupindukia.
Visababishi vya
Ugonjwa wa Kuvimba kwa Tezi ya Shingo
Chanzo kikuu cha kuvimba kwa tezi ni ukosefu wa
madini joto katika chakula na kutokea kwa maudhi mengine ya kihisia na kimwili
kunaweza kuliongezea tatizo Zaidi.
Chanzo kingine cha kuvimba kwa tezi ya shingo ni pamoja na mazoea ya
kula chakula kilichoondolewa uhalisia wake na ambacho hakikupikwa, pia ulaji wa
kupita kiasi wa vyakula vilivyopitia kiwandani na vilivyoondolewa ladha asili.
Soma pia MATIBABU YA ASILI YA UGONJWA WA KUVIMBA KWA TEZI YA SHINGO
Soma pia MATIBABU YA ASILI YA UGONJWA WA KUVIMBA KWA TEZI YA SHINGO
No comments:
Post a Comment