Utafiti wa hivi karibuni umefichua faida ya ndani ya kiafya
ya kitunguu swaumu itokanayo na mseto uitwao allicin uliomo katika kitunguu
hicho ambao ndio unaokifanya kiwe na ladha na harufu kali ya kunukia.
Wanasayansi waligundua kuwa mseto wa allicin huoza ili
kutengeneza sulfenic acid, ambacho ni ki-kemikali kinachochachamaa kupambana na
chembechembe za maradhi zinazoweza kusababisha saratani.
Vitunguu maji na vitunguu saumu vina miseto ya chumvichumvi
za kioganiki ambayo hujitokeza kusaidia msukumo wa damu na kupunguza
mabujabuja ya damu (blood clotting).
Nyanya
Hili ni tunda mashuhuri na lenye virutubisho ambalo kwa
kawaida hutumika kama mbogamboga. Kwa wastani,
watu hula takribani kilo 8 za nyanya kwa mwaka.
Nyanya zina aina mbalimbali za viasili vya kurutubisha na
visivyorutubisha vinavyohusiana na faida kadha wa kadha za kiafya.
Hii inajumuisha lycopene, vitamin C, A na K, potasiamu, na
nyuzinyuzi.
Nyanya moja yenye ukubwa wa wastani inaweza kutoa takribani
nusu ya kiasi cha kila siku cha vitamin C anachohitajika kupata mtu. Viasili mbalimbali vya nyanya vinasadikika
kufanya kazi pamoja kuleta manufaa ya kiafya.
Hii ni pamoja na kusaidia kujenga afya ya meno, afya ya
mifupa, afya ya ngozi, afya ya nywele, kupunguza shinikizo la
damu (BP) na kupunguza viwango vya lehemu pamoja na kupunguza hatari ya ugonjwa
wa moyo na saratani.
Baadhi ya vionjo vya nyanya kama vile lycopene hufyonzwa kwa
wepesi mwilini pale nyanya zinapochemshwa, iwe kwa kuzipika au kuzichemsha.
Sasa huenda tunazijua faida za kula lishe kamili ya kuleta
afya ikiwa ni pamoja na kula matunda na mbogamboga.
Lakini wasichokijua watu wengi ni kwamba juisi
ya mbogamboga ndiyo inayosaidia kudumisha urari (Ph) muhimu wa haidrojeni ya
mwili.
No comments:
Post a Comment