Jitihada za kuutibu ugonjwa wa vidonda vya tumbo
zimeshachukua muda mrefu duniani na kwa bahati mbaya, uhakika wa tiba bado
unaendelea kuwa kitendawili kisichoteguka hadi hii leo.
Hii ni kutokana na taarifa zinazozagaa kuwa vidonda vya
tumbo ni aina ya magonjwa ya kibakteria tu na kwamba, dawa za antibiotic
zinaweza kuutibu.
Kutokana na jambo hili ambalo limewafanya madaktari na
wagonjwa wabaki na sintofahamu ya muafaka wa kudumu.
Mwanzoni mwa karne ya 20, vidonda vya tumbo viliaminika kuwa
vilisababishwa na mgonjwa kuwa na “stress” zilizopitiliza pamoja na ulaji mbaya
wa vyakula ambavyo vilisababisha ugonjwa huu.
Hivyo kwa kulijua hilo, matabibu walitoa tiba dawa, kuwapa
mapumziko na kuwapa mpangilio maalumu wa chakula kisichoweza kuzalisha
tindikali tumboni mwa mgonjwa na kuamini kuwa hiyo ingekuwa tiba tosha, lakini
mafanikio yalibaki kuwa kitendawili.
Hakuna mtafiti aliyetulia tena toka hapo na hakika muda
mfupi tu ikagundulika kuwa tindikali inayozalishwa tumboni kwa ajili ya umeng’enyaji
wa chakula iitwayo ‘gastric acid’
ndiyo iliyozalisha vidonda vya tumbo na hapohapo dawa zenye uwezo wa kuzuia
tindikali hiyo isizalishwe tumboni mwa mgonjwa ikaanza kutolewa kwa mgonjwa.
Hii ilisaidia tu kupunguza idadi ya wagonjwa wa vidonda vya
tumbo duniani kwani dawa hizo zijulikanazo kama ‘antiacids’ zilisaidia sana
angalau kupunguza wagonjwa wa vidonda vya tumbo kulalamika kwa maumivu makali
wanayoyapata.
Ilipofika mwaka 1982, madaktari bingwa kutoka Australia, Dk.
Robin Warren na Dr. Barry Marshall walikuja na jibu la utafiti wao mpya kwamba
kumbe kuna bakteria waitwao ‘Helicobacteria pylori’ ndio wanaosababisha ugonjwa
wa vidonda vya tumbo na sio ulaji mbaya wa vyakula na stress.
Hata hivyo, habari hii ikaonekana kama inawachanganya
matabibu kwa kuwa tayari walishatumia dawa za antibiotics kutibu na
ikashindikana.
Hivyo mpaka hii leo madaktari na wagonjwa wengi bado
hawataki kuaminishwa tena kwamba vidonda vya tumbo vinaweza kutibika kwa
antibiotics na wengi hutumia dawa za mitishamba na tiba mbadala za aina tofauti zaidi kuliko kwenda hospitali kwa ushauri wa wataalam wa afya na dawa.
Bakteria hutokea wapi
Jibu la tafiti zangu binafsi linakuja kuwa stress humfanya
mtu asile chakula sawasawa na hivyo tindikali ‘gastric acid’ hushambulia kuta
za tumbo kwa ndani na kuzalisha vidonda vyenye bakteria hao.
Ila baadhi ya vidonda vya tumbo husababishwa na dawa kali
anazotumia mgonjwa kujitibu maradhi fulani, halafu unywaji wa pombe bila kula
na uvutaji wa sigara wa kupitiliza ni hatari sana!
Lakini ilipofika mwaka 1994, vyuo vya tafiti za magonjwa na
dawa vingi tu duniani vilithibitisha kuwa utafiti wa madaktari toka Australia
ulikuwa sahihi na kutoa mapendekezo kuwa wagonjwa waikubali tiba ya antibiotics
kwa kuwa hata wao walifanya tafiti na kujiridhisha kuwa bakteria wa
Helicobacter pylori walitibika kwa dawa hizo.
Mwaka mmoja baadae, rekodi zilionesha kuwa tayari asilimia 5
ya wagonjwa walishaanza kutumia antibiotics huku asilimia 75 ya wagonjwa
walibaki wakitumia tiba mbadala bila imani na antibiotics.
Hii ilikuja kubainika katika utafiti uliofanyika baadaye
kuwa asilimia 90 ya wagonjwa wa vidonda vya tumbo walikuwa bado hawajui kuwa
ugonjwa huo husababishwa na bakteria wa Helicobacter pylori.
Hivyo, ilipofika 1996, Mamlaka za vyakula na dawa duniani
zilitoa tamko rasmi juu ya matumizi ya aina maalum ya antibiotics kutibu
vidonda vya tumbo, lakini mpaka sasa muelekeo unaonekana kuwa na mafanikio
makubwa katika muda mfupi sana ujao.
Nani huugua
Vidonda vya tumbo ni ugonjwa unaoweza kumpata mtu yeyote
lakini watu wenye makundi kama haya ndio waathirika zaidi.
Kundi la kwanza ni wale wote waliothirika kwa bakteria wa H.pylori, pia, watu wenye mazoea ya
kumeza dawa za kutuliza maumivu mara kwa mara bila ushauri nao pia wako
shakani.
Ila, kama katika ukoo wenu kuna historia ya wagonjwa wa aina
hii, basi unaweza ukaupata pia, halafu wapo watu weye mazoea ya kunywa pombe
kupita kiasi bila kula chakula cha kutosha nao wamo hatarini.
Ukiachana na hao, watu waliowahi kuugua magonjwa yenye
uhusiano na mapafu, ini na figo pia huweza kuupata ugonjwa huu na kundi lingine
ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50, huweza pia kuupata ugonjwa huu japo
sio wengi.
Dalili zake
Dalili za vidonda vya tumbo ziko nyingi lakini sio lazima
zote mgonjwa azione ila baadhi ni lazima, nazo ni pamoja na kujisikia tumbo
linaongezeka gesi, huwezi kunywa kiasi kikubwa cha vinywaji na hata maji pia,
unapenda kukata kucha kwa meno mpaka unapatwa na vidonda vidoleni, ukila
hukawii kujisikia njaa tena, ukiamka asubuhi unajisikia kichefuchefu, kujisikia
mchovu nakujihisi kuumwa na kukosa hamu ya kula.
Ukiona dalili hizo unatakiwa ukamuone daktari haraka kwani
ukichelewa kuidhibiti hali hiyo basi utajikuta ukitapika mara kwa mara na pengine matapishi yakawa na damu, au unaweza kupata kinyesi cheusi na chenye
kunata na muathirika anaweza kujisaidia kinyesi chenye damu, hali ambayo
inaonesha kuwa hali tumboni mwa mgonjwa sio shwari tena.
Nini cha kufanya?
Kwa kawaida, vidonda vya tumbo visivyo vikubwa hupona
vyenyewe hasa kwa watu wenye kinga thabiti ya maradhi. Hali hiyo haizuii kwa muathirika kwenda
haraka hospitali kumuona daktari ambaye atachukua vipimo na kujua kitu gani
kifanyike kwa ufasaha zaidi.
Lakini wakati unafanya hivyo, jaribu kunywa dawa za
kupunguza tindikali tumboni ambazo hata daktari anaweza akakuandikia kwa kuwa
tindikali ikizidi tumboni basi hata maumivu pia huzidi kwa mgonjwa na hata vidonda
huzidi kutanuka.
Kitu kingine cha muhimu kufanya ni kuacha kutumia dawa
zozote za kutuliza maumivu kama aspirini na Panadol au Ibrupfenol bila
kushauriwa na daktari.
Usinywe maziwa
Watu wengi hushauri kunywa maziwa kwa kuwa hutuliza maumivu
ya vidonda vya tumbo kwa kuziba kuta za ndani ya tumbo kwenye vidonda, lakini
hiyo huwa kwa muda mfupi na hatimaye maziwa hayohayo yatachochea uzalishaji wa
tindikali kwa wingi tumboni na kufanya vidonda visipone.
Kunywa juisi ya kabichi walau glasi moja kila siku. Muombe daktari akuandikie multivitamin yenye
vitamin D kwa wingi kwa kuwa ukitumia itasaidia kukausha vidonda kwa haraka.
Tumia pilipili
Pilipili ni dawa nzuri japo wapo wanaopinga hilo kwa madai
kuwa itaongeza maumivu na kukuza vidonda, huo ni uongo!
Tafiti nyingi zilizofanyika duniani zinaonesha kuwa pilipili
hufukuza bakteria katika vidonda na pia humuongezea mgonjwa madini ya chuma
ambayo humfanya mgonjwa awe imara na apate nafuu haraka ila dawa za kutuliza
maumivu zinahitajika unapotumia pilipili.
Kitalaamu, hakuna aina ya chakula ambacho
kikiliwa huwa hakizalishi tindikali wakati wa kufyonzwa na kuta za tumbo hivyo
kula vyakula vyenye tiba ndio kitu cha msingi na maana.
Mkuu kuna uthibitisho wa waliopona
ReplyDelete