Kuusafisha mfumo wa
damu
Matibabu ya uvimbe wa tezi ya shingo yanapaswa kuanza kwa
kuusafisha mfumo wote wa damu na kuanzisha matumizi ya mlo unaostahili pamoja
na utulivu na mapumziko ya kutosha. Kwa
kuanzia maji ya matunda kama vile Matufaa maji (Apple), zabibu, mananasi, na
machungwa yanapaswa kunywewa kwa mpishano wa masaa mawili na nusu kwa muda wote
wa siku kwa siku nne.
Kujiinika
Kujiinika kwa maji ya uvuguvugu kunapaswa kufanywa kila siku
kwa kipindi hiki chote ili kusafisha njia ya haja kubwa.
Kutumia Mlo Unaostahili
Baada ya hatua ya kujiinika, mgonjwa anapaswa kuanza kutumia
mlo wa maziwa na matunda, akipata milo mitatu kwa siku ya matunda yenye maji
kama vile matufaa, mapapai na zabibu yakiwa pamoja na glasi ya maziwa kwa
mpishano wa masaa matano.
Mgonjwa anaweza kubadili taratibu mlo wake na kuanza kutumia
mlo ulio na virutubisho kamili. Katika
utaratibu huu anapaswa kula matunda yaliyo katika hali ya upya wake (fresh),
yasiyo na muda mrefu tangu yachumwe.
Matunda hayo yanapaswa kuwa matufaa (Apples), Machungwa, zabibu,
mapeasi, na madalanzi, jamii za karanga zilizo mbichi na glasi ya maziwa
yasiyochekechwa kuondolewa mafuta vitumike asubuhi. Chakula cha mchana kinapaswa kuwa mboga za
majani zilizochemshwa au kupikwa bila kuiva, chapati zilizopikwa kwa ngano ya
atta isiyokobolewa na glasi ya maziwa mazito yasiyochekechwa mafuta. Supu ya mboga za majani, saladi za mboga
mbichi za majani kama vile nyanya, karoti, letusi, kabeji, celery na
tanipu. Mbegu za Alfalfa, jibini ngumu
iliyotengezwa kienyeji na jamii zote za karanga zikiwa katika ubichi zitumike
wakati wa usiku. Glasi ya juisi ya
matunda au maziwa inywewe kabla ya kwenda kulala usiku. Vinywaji kama chai, kahawa, unga uliokobolewa
na vyote vinavyotengezwa kwa ngano nyeupe, sukari nyeupe, vyakula vyenye mafuta
mengi, nyama yenye mafuta, vyakula vya kiwandani, na achari za kiwandani
vinapaswa kuepukwa kabisa na mgonjwa wa uvimbe wa tezi ya shingo.
Mapumziko ya Kutosha
Mgonjwa pia anapaswa kupata muda wa kutosha kupumzika, iwe
angalau siku nzima kwa kila wiki kwa miezi miwili ya mwanzoni ya matibabu.
Mazoezi
Pia ni vyema kwa mgonjwa kuanza kufanya mazoezi ya kutosha
pale dalili za ugonjwa huu zikianza kupotea.
Mengine ya Kuzingatia:
Madini ya Joto
(Iodine)
Vyakula vilivyo na madini joto kwa wingi vinapaswa kutumika
bila kipimo kwa muda wote kwani humsaidia mgonjwa kupona haraka. Vyakula hivi ni pamoja na mboga za majani
kama vile Kabeji, vitunguu swaumu, asparagus, oats, karoti, vitunguu na nyanya,
strawberries, na mchele usiolowekwa.
Kutumia Maji
Pamoja na hatua hizi, tiba nyingine za kutumia maji zina
manufaa katika kuondoa uvimbe. Hii ni
pamoja na kuukanda mwili wote kwa maji kabla ya kwenda kulala na kuukanda mwili
wote kwa maji ya baridi unapoamka asubuhi inasaidia pia. Endapo ukosefu wa choo utakuwa unajitokeza
mara kwa mara, hatua zote muhimu zinapaswa kuchukuliwa katika kuliondoa tatizo
hilo.
Kuondoa mawazo
Pia mgonjwa anapaswa kujaribu kuliondoa tatizo la msongo wa
mawazo na wasiwasi katika maisha yake ya kila siku. Katika hatua za mwanzoni, kunaweza kuwa na
kujirudia kwa dalili za mwanzoni lakini zitakuwa zikijionesha kwa muda mfupi na
katika hali isiyo kali sana na kudumu kwa muda mfupi kadri tiba itakavyokuwa
inaendelea. Kikubwa ni kuwa mgonjwa
anapaswa kuwa na mtazamo chanya juu ya kupona kwake kwani ndio msingi wa
kufanya kazi kwa mafanikio.
Kutokana na yaliyooneshwa hapo juu, utaona kuwa
ugonjwa huu unatibika bila shaka yoyote kwa kutumia vitu vya asili kabisa.
No comments:
Post a Comment