Kila mmoja amewahi kuhisi tumbo kujaa wakati wote, hali hii
hutokea mara kadhaa kwa nyakati tofauti.
Japo ni hali ambayo kwa kawaida inatokana na ulaji kupita kiasi, lakini
kuna baadhi pia hawana tabia ya kula kupita kiasi bado wanakumbana na hali
hiyo.
Hivyo ni vyema tukafahamu kuwa, sambamba na tabia za ulaji,
kuna sababu zingine zinazochangia hali hii kama vile mwili kuhifadhi kiwango
kikubwa cha maji.
Pia inaweza kutokana na matatizo mengine ya kiafya kama vile
dalili ya vidonda vya tumbo ambayo huambatana na uwepo wa gesi tumboni na hivyo
kuongeza ujazo wa tumbo na matatizo mengine yanayojitokeza kwenye mfumo wa
chakula.
Zifuatazo ni sababu nyingine zinazochangia kwa kiasi kikubwa
sana kujaza tumbo na kusababisha kero kwa walio wengi.
“Premenstrual
syndrome” hili ni jina la kitaalam linalotafsiri baadhi ya matatizo ya
kiafya madogo kama vile uchovu, maumivu na hata kichefuchefu yanayojitokeza kwa
mwanamke wakati akikaribia kuingia kwenye mzunguko wa hedhi.
Premenstrual syndrome pia inasababisha mwili kuhifadhi
kiwango kikubwa cha maji kutokana na mabadiliko ya mfumo wa homoni kwa wakati
huo.
Hivyo, ndani ya kipindi, ni kawaida kwa mwanamke kuhisi
tumbo lake limejaa wakati mwingi.
Ulaji wa chumvi kwa wingi ni moja ya sababu hizi. Ni dhahiri kuwa miili yetu inahitaji chumvi,
lakini mara nyingi tumejikuta tukitumia zaidi kiwango stahiki kinachostahili
kuingia mwilini.
Chumvi ikizidi mwilini inaupa mfumo wa mwili kuhifadhi
kiwango kikubwa cha maji na chumvi pia inaweza kusababisha matatizo mengine
makubwa ya kiafya kama vile shinikizo la juu la damu.
Kwa siku za karibuni, matumizi ya vyakula vilivyosindikwa
yameongezeka maradufu, ni muhimu kuzingatia kuwa asilimia kubwa ya vyakula
vilivyosindikwa vimewekwa kiasi kikubwa cha chumvi na hata kama usipohisi ladha
ya chumvi kwenye vyakula hivyo haina maana kuwa havijawekewa chumvi.
Unywaji wa soda na vinywaji vingine vya kiwandani pia
unachangia sana kulifanya tumbo muda wote liwe limejaa kama soda na vinywaji
vingine kama bia, shampeni na vingine vyenye gesi.
Unapokunywa moja ya vinywaji hivi vinaenda kuongeza ujazo
kwenye mfumo wako wa chakula. Wakati ukiendelea
kunywa, unaweza kutoa kiasi kidogo cha gesi, wengi wamezoea kuita kudukua au
kubeua. Hii inatokea pale unapokunywa
kinywaji chenye gesi na ghafla inakujia hali kama unacheua hivi, lakini
kinachotoka ni gesi.
Hii haimaanishi kuwa kwa kufanya hivyo, gesi yote uliyoipata
kutoka kwenye kile kinywaji imetoka, hapana.
Kiasi kikubwa cha gesi hiyo huendelea kubakia kwenye utumbo wa chakula.
Ikumbukwe kuwa, karibu soda zote zimewekewa sukari kwa wingi
sana na huenda kiwango cha sukari kilichopo kwenye soda kinazidi kiwango
kinachostahili kuingia mwilini, hivyo sukari hii inapoingia mwilini
inaulazimisha mwili kuhifadhi kiwango kikubwa cha maji kwenye mfumo wa
chakula na mbaya zaidi unajiweka kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa ya
kisukari.
Tafadhali zingatia kuwa, sio baadhi tu ya soda,
bali soda karibu aina zote zinaweza kukuletea madhara haya. Pia kukosa haja kubwa ni sababu nyingine
inayochangia tumbo kujaa. Ulaji vyakula
ambavyo havina nyuzi lishe, na hata msongo wa mawazo ili kuweza kukabiliana
nazo.
No comments:
Post a Comment