Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni:
1. INTROVANT: Watu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa
kina, katika eneo hili hapa kuna makundi mawili nayo ni;
I.Melancolin
II.
Fragmetic
2. EXTROVANTS: Wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za
kina katika mambo yao Hapa pia kuna makundi mawili nayo ni;
I. Sanguine
II.
Colerick
Sasa tuangalie tabia za kila kundi na mienendo yao
1. MELANCOLIN: Watu
wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo -wana uwezo mkubwa
kiakili (high intelligence Quotient) -ni wagunduzi wa mambo makubwa ya
kisayansi -wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu -ni watu wenye pole pole
na wasio na maneno mengi -wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika
kuwa na upendo wa dhati -Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na
matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)
-Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa -Wanajitolea kwa haraka
na kwa dhati katika mambo ya wengine -Huondoa uchungu wao kwa machozi
(wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana) -Hawajiamini
kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasanu si wepesi wa kunyoosha vidole ili
kujibu maswali) -Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka
kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje
kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia
katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo) -Wakata tamaa
wanapokosolewa. -Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia. -Wanapenda kusoma,
kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi
umbea) -Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa
wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama
mahubiri hayo -Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika. -Wanapenda
usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao -Ni wa vumilivu sana katika hali
mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa) -Hawapendi kufuatilia mambo ya
wengine pasipo sababu za msingi. -Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na
magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana -Ni wagumu wa kusahau na
hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe -Wanaumia sana wanapokosea ama
kushindwa jambo Fulani -Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo
wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyoni mwao) -Wana busara na hekima nyingi -Ni watu ambao wakiishika imani fulani
wanajitahidi kuitimiliza sheria yote. -Ni wepesi wa kutubia makosa yao na
kutubu kwa ajili ya wengine. -Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu
wala kuzoeana nao -Ni kundi la watu wanoridhika haraka -Masikini wengi kiuchumi
duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo
kwa kuhofia kushindwa -Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni
wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza
kutimiliza ndoto zao kutokana na uoga wa kuanzilisha mambo mapya. -Kundi
linalopenda amani na utulivu -Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
-Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto
kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu -Mara
nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
-Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi -Ni kundi la watu wenye
marafiki wachache -Wakati mwingine hupenda kujikataa. -Ni waaminifu na wasema
ukweli -Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao -Ni waaminifu sana kwa
mambo ya kawaida na yale ya kiimani -Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya
watu -Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda
kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba
kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni
melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick -kingine kinachowanyima
sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja
zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili,
alikuwa hajiamini, anakata tamaa mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha
ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa
nchi ya ahadi-Kaanani] -Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo
wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno} -Kwa
upande wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu
ya hedhi, na kujifungua
2: FLAGMETIC -Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya
melancolin -Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia
moja na sitini -Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda
kupalilia shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe
na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia) -Wanapenda sana kupuuzia
mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe -Hawapendi kukubali
ama kusifia mafanikio ya wenzao -Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni
mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea -Katika ushindani hasa wa hoja
huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja
akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande) -Mawakili majaji
na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili -Ni watu
wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao
mengi hutawaliwa na mifano na takwimu halisia -Wanapenda kufuatilia mambo ya
wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu) -Wapelelezi
mahiri hutoka katika kundi hili -Ni watu wasioumizwa kufanya makosa -Hawapendi
kuwaamini wenzao -Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea
kwa mambo mbalimbali -Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa
uhakika -Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza
kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro
katika ndoa zao) -Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)
-Ni wagumu wa kuomba msamaha (i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi)
ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi
sana kuamka) -Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera,
vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera walizozipokea -Si watu wanaojali
muda na ratiba -Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua
kusalitiwa ama kurubuniwa. -Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni
hadharani -Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao -Ni wasuluhishi wazuri wa
migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya
utele kwa neno la upatanisho ipo kwao) -Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini
kwa ufanisi wa wastani -Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya
usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu) -Wakianzisha jambo huweza
kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko -Ni watu
wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama -Wapo
tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani
(wanafahamika kama peace makers) -Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona
wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote -Hawapendi kuelekezwa na mara
nyingi eidha huwadharau viongozi wao ama hutengeneza mitazamo na hoja za
kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao. -Wanapenda kutekeleza
maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuia -Wakiwa viongozi huweza
kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja
na matakwa ya wale wanaowaongoza.
3.SANGUINE -Wana uwezo wa kawaida kiakili
(mara nyingine mdogo) -Ni wacheshi sana -Watu walio na maneno mengi na
wasiopumzika kuongea -Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu
wengine wakiwasikiliza -Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine
-Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika kundi hili -Wanapenda sana
kujisifu na kujikweza -Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana
uhalisia -Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya.
-Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo
huvionesha kwa uhakika -Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na
kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na
kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama
ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine)
-Muda wote wako nadhifu (ni wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu) -Wana
kiherehere sana. -Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau -Ni vinyonga katika
tabia zao (wana uwezo wa kuigiza tabia zisizo zao kiuhalisia na watu wasiowajua
wasiwagundue kirahisi) -Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini
ni rahisi kuyaacha -Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa
silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi -Ni kundi
linaloathiriwa sana na love affairs (i.e wao ni multiple lovers-ni kawaida
kumkuta sanguine akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja: __inasemekana kutokana na maneno
yao mengi na ufundi wa kuigiza hisia na tabia wavulana wanaume wa kundi hili
huwanasa wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa.) -Wawapo kwenye jamii
hukubalika sana hasa kutokana na ucheshi wao na ukarimu walio nao. -Wanapenda
sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha -Ni wahamasishaji wakubwa na
wenye ushawishi wenye kukubalika kirahisi -Ni kundi la wainjilisti wanaoongoza
kwa kurudisha kondoo wengi kwa Bwana (wengi wana karama za kuhubiri kwa mvuto
na ushawishi wa pekee) -Hawaumii wanapokosolewa, ama wanaposhindwa jambo -Ni
kundi la watu waoga sana (wanajiamini sana kwa maneno lakini kivitendo ni
kunguru) -Si watunzaji wazuri wa siri (waropokaji) -Wanapenda kujaribu kila
jambo linalokuja mbele yao -Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko wengine
-Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine -Hawana aibu hata mbele ya watu
wasiowafahamu wala kuwazoea -Wanaume wa kundi hili huamini kuwa walizaliwa kwa
ajili ya kuwasaidia wanawake -Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe
na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala (wanapenda kuwaza
jinsi ya kupata bahati nasibu, kuzawadiwa fedha na hata kuokota fedha ama
madini) -Ni watu wasiojua namna ya kupanga na kuimudu bajeti kwa ustadi) -Ni
watu wa mipango isiyoona mbali (wakurupukaji) (Ministers of emmergency affairs)
-Ni wazuri katika kusifia(i.e wanazikubali kazi za wengine kirahisi na kwa
dhati) -Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na hivyo kuwa maarufu
-Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina. Mfano ni
Petro mtume wa Biblia: alipenda kujaribu kila kitu (alipomwona Yesu anatembea
juu ya maji alitaka na yeye kufanya hivyo) alipenda kufahamu kila kitu
(aliuliza habari za siku za mwisho) alipenda kujionesha kuwa ni jasiri
(aliahidi kuteswa na Yesu), alikuwa ni muoga sana (alimkana Yesu mara tatu kwa
kuhofia kuteswa na wayahudi), alikuwa ni mwinjilisti wa kutumainiwa (alihubiri
siku ya Pentekoste), alikuwa ni mwepesi wa kukubali pindi anapokosolewa
(alikiri makosa baada ya kuonywa na Paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri
kuwa hakuna wokovu kwa wasiotahiriwa)
4. COLERICK -Wana uwezo wa kawaida
kiakili -Ni wa wakali na wakaidi -Hawana huruma wala unyenyekevu -Watu
wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa -Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote -Ni
viongozi kwa asili ya kuzaliwa -Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa
-Watu wasiokata tamaa mapema -Wanajiamini kupita kiasi -Hawana uoga ni majasiri
sana -Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
-Kundi la watu wenye nguvu nyingi -Ni madikteta -Hawapendi kabisa kupingwa wala
kukosolewa -Watu wa kulipiza visasi -Watu wa vitendo kuliko maneno -Ni waonevu,
wanapenda dhuruma na ubabe -Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
-Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo
lenye upinzani eneo fulani -Wanafaa sana kuwa viongozi kutokana na uhodari wao
wa kuwaongoza watu kwa sera za ushawishi wenye mlengo -wa kiukandamizaji
-Hawajui kubembeleza -Hawaongei wala kucheka ovyo -Wanapotenda jambo huwa
wanawaza namna ya kunufaika na hata kama akimsaidia mtu anawaza namna ya
kurudishiwa hicho alichokitoa -Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa
kutokana na uimara wao katika kuthubutu kutenda mambo na hali zao za kutoogopa
hasara -Si watu wanaopenda suluhu na amani -Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
-Hawapendi starehe kwa wingi -Ni watu wanaoweza kufurahia mazingira yenye dhiki
na shida -Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe
hata baada ya kufariki -Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na
filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha -Mifano ya watu wa kundi hilo: Idd
Amin, Hitler, etc *SI TABIA ZOTE ZA KUNDI LAZIMA ZIANGUKIE SEHEMU MOJA. MAMBO
MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU -Kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe
katika kundi fulani -Huwezi kujibadilisha kundi -Kujifahamu kundi lako
kunakuwezesha kurekebisha madhaifu uliyonayo na kuimarisha mazuri uliyonayo.
Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kuwa makini namna ya kuishi nao
-Inawezekana kabisa kujifahamu upo kundi gani na pia kwa kusoma na kutazama ni
rahisi kutambua makundi ya wengine *NITATAMBUAJE MIMI NI WA KUNDI GANI? -Watu
wengi wana tabia za makundi zaidi ya moja-Kwa wale tabia zaidi ya asilimia
themanini kutoka kundi fulani hao wanaitwa pure (i.e pure sanguine etc)-Kama
una tabia kutoka kundi zaidi ya moja, unaunganisha majina ya makundi mawili
yenye tabia nyingi zaidi, unaanza jina la lile lenye asilimia nyingi zaidi.
*Mfano: flag-coleick; cole-flagmetic, flag-colerick , sangu-melancolic,
melanco-sanguine: etc
No comments:
Post a Comment