Thursday, May 14, 2015

CHAKULA KWA AJILI YA MAISHA YOTE

Chakula kisichokobolewa huimarisha miili yenye afya! Kifurahie!

Tuchukulie umetoka kununua gari uliyokuwa unaitamani sana: aina ya Porsche Panamera, Mercedes-Benz S-Class au Audi A8.  Unadhani unaweza kufikiria kutumia mafuta ya hali ya chini kabisa, kupuuza kubadilisha oili, au kupuuza kabisa maelekezo ya watengenezaji yaliyotolewa katika maelekezo ya utunzaji?  Bila shaka hapana!  Kama umetoka kulipa zaidi ya shilingi 144,000,000 kwa ajili ya gari la kifahari, utakuwa makini sana katika kuliweka katika hali nzuri kabisa.

Mwili wa binadamu ni mzuri, ni changamano na umeundwa kwa umakini kuliko gari lo lote ulimwenguni.  Miili yetu inaonesha uhandisi na akili ya ajabu kabisa.  Fikiria maajabu ya seli moja, uchangamano wa ubongo, uchangamano makini wa moyo au mwujiza wa uzazi toka kwa Mungu.  Tunashangazwa na ubunifu makini wa mwili wa mwanadamu.  Mwumbaji mwenye upendo alifanya kila njia kutuumba na kama lilivyo gari la kifahari miili yetu pia inahitaji fueli (mafuta) bora kabisa ya kuendesha maisha yetu, na fueli hiyo inatokana na vyakula tunavyokula.  Bila fueli (mafuta) ya hali ya juu katika gari la kifahari, gari huenda mwendo mfupi zaidi kwa kilometa, hupoteza nguvu, na injini huwa haitembei vizuri.  Na bila lishe sahihi, miili yetu pia haiwezi kufanya kazi sawasawa.

Lishe yenye ulingano iliyochaguliwa kutoka katika vyakula bora itatoa virutubisho muhimu kwa ajili ya ukuaji, ukarabati na nguvu.  Tunapochagua vyakula duni au tusipokula kiasi cha kutosha, mashine ya mwili huteseka.  Na tukila kupita kiasi vyakula vilivyokobolewa na kusafishwa sana, tunaweza kunenepa kupita kiasi kwa urahisi na kukosa virutubisho muhimu.  Aliyetuumba anajali kuhusu afya zetu na inatupasa sisi tujali pia, “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo” (3 Yoh. 2).

Kutunza miili yetu si jambo la ziada.  Ni jambo lililo katika moyo wa Mungu.  Usije ukachanganya mambo.  Hatuwezi kwenda mbinguni kwa ajili ya namna tunavyokula.  Tunaokolewa kwa neema, na neema peke yake (Efe. 2:8).  Hata hivyo, tunaweza tukashindwa kutimiza makusudi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu kwa sababu ya mazoea yetu mabaya katika ulaji wetu.  Usijidanganye: tunachokula ni muhimu.
Share:

No comments:

Post a Comment