Maharage ya
soya yana protini nyingi zaidi ya nyama na mayai. Protini ndani ya Soya ni asilimia 36.5, nyama
ina asilimia 20 na mayai asilimia 12.
Soya pia ina mafuta, wanga na vitamini B na E. Madini muhimu kwa afya ya binadamu kama vile
chuma, potassium, copper, zinc na manganese nayo yanapatikana katika chakula
hiki. Soya pia ina nyuzinyuzi za chakula
pamoja na dawa-lishe kama vile phytoestrogen.
Soya
husaidia katika kinga ya ugonjwa wa saratani ya matiti na ile ya tezi
dume. Hurekebisha vichocheo vya jinsi na
mzunguko wa hedhi na kupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi kwa
wanawake. Hii ni kwa mujibu wa utafiti
uliochapishwa mwaka 1994 katika jarida la American Journal of Clinical
Nutrition toleo la 60.
Pia huimarisha
afya na nguvu za tendo la ndoa kwa jinsi zote, hii ni kutokana na L-arginine
inayopatikana ndani ya soya. Inasaidia
mama anayenyonyesha kupata maziwa kwa wingi, kwa vile huchochea uzalishaji wa
homoni ya prolactine inayohusika na uzalishaji wa maziwa. Soya pia huimarisha
mifupa, afya ya moyo na mishipa ya damu kwa kuzuia ugonjwa wa kusinyaa kwa
mishipa ya damu. Hushusha kiwango cha
lehamu mbaya mwilini na kuifanya damu kuwa nyepesi; kwa namna hiyo husaidia kuzuia
magonjwa ya shinikizo la damu na kiharusi.
No comments:
Post a Comment