Huwa
tunaichochea miili yetu kwa vyakula tunavyochagua kula. Huwa vinatoa virutubisho muhimu kwa ajili ya
maisha ya afya na yenye manufaa. Usagaji
wa chakula ni mchakato tata wa kuvunjavunja chakula kuwa tofali moja moja ili
mwili uyabadilishe na kuyatumia kuendeleza uhai. Mchakato huu huanzia mdomoni, kwenda tumboni,
kisha kwenye utumbo mwembamba na hatimaye kwenye utumbo mpana.
Tunaweza kugawa
virutubisho katika kategoria au makundi haya muhimu:
Ø Kabohaidreti: Katika mlo bora, sehemu kubwa ya kabohaidreti haina budi
kutoka katika vyanzo bora visivyokobolewa/kusafishwa, kama vile nafaka, jamii
ya kunde, matunda, na mboga.
Ø Protini:
Kila seli mwilini ina protini.
Ukarabati wa tishu na ukuaji unazihitaji. Wakati kila chakula kina protini kiasi fulani, mazao ya wanyama kama vile maziwa na mayai ni vyanzo vizuri pia, lakini si vyanzo pekee. Jamii ya kunde zina
protini bora kabisa.
Ø Shahamu: Hivi ni vyanzo vilivyosheheni nishati. Mara nyingi tunakuwa na mafuta mengi kupita
kiasi katika milo yetu kwa sababu ya ladha ambayo mafuta hukipatia
chakula. Watu wengi huona ni bora wale
chipsi kuliko viazi vya kuchemsha. Hata
hivyo, vyakula vya jamii ya karanga vikiliwa kwa kiasi hutoa mafuta bora. Mwili unahitaji mafuta kama hayo ili ufyonze
vitamini zinazoyeyuka katika mafuta.
Ø Vitamini: Sehemu asilia ambazo ni muhimu katika chakula, na
zinahitajika na kiasi kidogo kwa ajili ya ukuaji wa kawaida na utendaji
kazi. Vitamini nyingi hupatikana kwa
asili katika vyakula mbalimbali. Zingine
huyeyuka katika maji na zingine katika mafuta na tusipopata za kutosha ugonjwa
utokanao na upungufu hutokea.
Ø Madini: Elementi hizi zisizo hai ni muhimu kwa afya ya mwanadamu na
hupatikana kwa urahisi katika vyakula vitokanavyo na wanyama na vile
vitokanavyo na mimea. Chache sana kati
ya hizo zinaweza kuleta ugonjwa utokanao na upungufu.
Ø Antioksidanti na Faitokemikali: Sasa, wanasayansi wanatambua mamia ya vitu hivi, mbavyo
hulinda mwili dhidi ya magonjwa na baadhi ya athari za uzee. Huwa tunazipata katika nafaka zisizokobolewa,
matunda, mboga na jamii ya karanga.
Unahitaji kategoria au makundi yote haya ya chakula ili uwe na afya bora. Siri ipo katika uchanganyaji
No comments:
Post a Comment