Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya
afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa
njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na
vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la
chips.
Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama
dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula
mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri.
Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na
mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai.
Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo
unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka
kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza.
Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale
yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaiva nusu.
Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu.
Hata ukienda kwa wakaanga chipsi, utakuta wanawauliza wateja wao
kama wanapokaanga na mayai wakaushe au wasikaushe. Hii inaashiria kuna watu
wanataka wale chipsi zikiwa na mayai ambayo halijaiva sawasawa.
Kuna watu wengine wanaamini kwamba kula mayai mabichi kunafanya
sauti inakuwa nyororo, hivyo wale waimbaji huwalazimu kufanya hivyo ili kufanya
nyimbo zao zivutie.
Si hivyo tu, kuna baadhi ya watu huamini pia dawa ya kikohozi ni
kunywa yai bichi lililochanganywa na asali. Hizi ni imani ambazo zimejengeka
kwenye jamii na watu hufanya hivyo ili kufikia malengo waliyokusudia.
Katika siku za karibuni, imevuma kuwa mayai ya kwale yanatibu
magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na kifua.
Katika mpango huo, wanapendekeza wahusika kula mayai mabichi ya
kwale tena kwa kutafuna hadi kaka lake, yaani ganda la nje.
Hali hii imesababisha biashara ya mayai ya kwale kuwa kubwa na
hata wafugaji wameongezeka mara dufu.
Wataalamu wanasemaje?
Mhmh
ReplyDelete