Tatizo la
unene uliokithiri limeongezeka sana kiasi kwamba wataalamu wa afya wameanza
kuliita gonjwa la mlipuko. Ugonjwa wowote ukizidi katika jamii au
eneo fulani, sayansi ya tiba huliita janga, lakini ikitokea katika sehemu
nyingi za ulimwengu kwa wakati mmoja pia huliita janga.
Kulingana na
shirika la afya ulimwenguni, kwa uchache watu milioni 2.8 hufa duniani kote
kila mwaka kwa sababu ya kunenepa kupita kiasi.
Tatizo hili lipo katika nchi tajiri na maskini pia. Unene kupita kiasi si suala la jamii zenye
kipato kikubwa tena.
Unaweza
kukokotoa kiwango cha unene, ambao huelezewa kama usio wa “mrundikano mkubwa au
uliokithiri wa shahamu unaoweza kudhuru afya,” kwa kutafuta kiashirio cha uzito
wa mwili wako (Body mass index [BMI]).
Kufanya hesabu hiyo, gawa uzito wako katika paundi kwa kipeo cha pili
cha urefu wako katika inch kisha zidisha kwa 703. BMI yako 25 au zaidi, una uzito mkubwa, na
kama ni 30 au zaidi, una ugonjwa wa kunenepa kupita kiasi. Kwa hali zote mbili, ni vyema kuanza program
ya kubadili mtindo wa maisha.
Kwa kifupi
fomyula katika vipimo vya metriki ni: BMI = (uzito katika kilo) / (urefu katika
mita x uzito katika mita). Kwa mfano,
kama uzito wako ni kilo 60 na una urefu wa mita 1.70, BMI itakuwa BMI =60 /
(1.7 x 1.7) = 20.8 (upo katika kategoria ya kawaida).
Kama hutaki
kuhangaika na mahesabu, ingia tu katika intaneti upate kikokotoo cha BMI. Utapata vingi, vya vipimo vya kiingereza na
vya metriki.
BMI
inaashiria nini? Je, uko hatarini? Je, una uzito mkubwa? Shinikizo la damu yako ni la kawaida? Je, unakula mafuta mengi, karoli, au vyakula
vilivyokobolewa na kusindikwa? Je,
chakula chako cha kawaida hutoka katika migahawa ya chakula cha haraka? Kama ni hivyo, uko hatarini, au tayari
unaweza kuwa na matatizo ya kiafya na hujui.
Vyombo vya habari hutangaza njia nyingi “za
ajabu” za kupunguza uzito, lakini njia bora kuliko zote ni badiliko kubwa la
mtindo wa maisha.
No comments:
Post a Comment