Kitambi ni nini? Haya
ni mafuta yaliyozidi kuzunguka eneo la tumbo.
Kinaweza kutokea kwa watoto, vijana na watu wazima hata wazee wa jinsia
zote.
Mwili wa binadamu una seli bilioni 50-200 za mafuta zilizogawanyika
kwenye mwili wa binadamu. Kwa wanawake
zipo sana maeneo ya matiti, nyonga (hips), kiunoni na kwenye makalio. Kwa wanaume seli zipo sana kwenye kifua,
tumboni na kwenye makalio.
Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu
mbili, ya kwanza, ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi na ya
pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo na kongosho.
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa
nguvu (kalori) kama vile mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi
anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.
Sababu zingine ni kuwa na chembe za urithi za unene kutoka
kwa wazazi. Kuna sababu za kimazingira
na nyingine zisizojulikana.
Vitu kama kukosa usingizi na sababu nyingine zinachangia
kuendelea kuwepo kwa kitambi ambacho kinaweza kuashiria maradhi ya moyo,
kisukari na baadhi ya magonjwa ya saratani.
MCHANGANUO WA SABABU 10 ZINAZOFANYA MTU KUENDELA KUWA NA KITAMBI
1. Unaanza kuzeeka
Kadri unavyozeeka, mwili wako
unabadili jinsi unavyo ongezeka na kupunguza uzito. Jinsi zote; za kike na kiume, hupatwa na
kupungua kwa utendaji wa kimetaboliki, kutia ndani kiasi cha kalori
zinazohitajika kwa mwili kufanya kazi kwa ukawaida.
Zaidi ya hayo wanawake hupatwa na
kukoma kwa hedhi, ikiwa wanawake wataongezeka uzito, mara nyingi uzito huo huwa
kwenye matumbo yao. “Profesa Michael
Jensen wa kliniki ya moyo alisema.
Wakati wa kukoma kwa hedhi, uzalishaji wa homoni za Instrojeni na
Projesteroni hupungua. Wakati huohuo
homoni ya testosterone huanza kupungua kidogo kidogo. Mabadiliko ya homoni hufanya wanawake wengi
kuendelea kubeba uzito mwingi kwenye matumbo yao.
2. Kutofanya mazoezi kwa usahihi
Mazoezi ya kulala chali na kuinua mwili
kuanzia kiuno hadi kichwa (Crunches) sio mazoezi yatakayokusaidia kuondoa kitambi. Badala yake fanya mazoezi ya
stamina yatakayokufanya utumie nyama (muscles) za tumbo, mgongo, nyonga na
sehemu zingine za mwili. Kufanya mazoezi
ya namna hii kutasaidia kuunguza/kutumia kalori nyingi mwilini na hivyo kufanya
mafuta yaliyo maeneo ya tumbo kutumika pia.
Mazoezi ya kukaa kwa muda jinsi fulani kama
unapiga pushap kitaalamu inajulikana kama plunk, ndio mazoezi yanayofaa kwa
kuwa huhusisha matumizi ya nyama za mikono, miguu na makalio.
Kukimbia kila siku ni mazoezi bora kwa
mwili na moyo wako ingawa mazoezi kwa ajili ya moyo wenye afya peke yake
hayawezi kusaidia maeneo ya kiunoni kutia ndani kitambi.
“unahitaji kufanya mazoezi ya kuondoa uzito
pamoja na ya kuweka moyo wenye afya.”
Anasema Dk. Sangeeta Kashyap wa kliniki ya Cleveland.
“mazoezi ya kutafuta stamina huongeza
ukubwa wa nyama za misuli kitu kinachofanya mwili wako kuunguza/kutumia mafuta
kwa sana na kuondoa kitambi.” Anasema
Kate Patton, mtaalamu wa lishe wa kliniki ya Cleverland. Patton anapendekeza dakika 250 za mazoezi ya
kawaida au dakika 125 za mazoezi magumu kila wiki.
3. Una mkazo
Kuwa na majukumu mengi ya kikazi, familia,
kulipa gharama za shule na bili mbalimbali kama umeme na maji kunaweza kufanya
ugumu katika kupunguza uzito usiotakiwa mwilini, hasa kuanzia umri wa
kati. Homoni ya mkazo iitwayo Cortisol
huongeza kiasi cha mafuta kinachochukuliwa mwilini na kutanua seli za
mafuta. Uwepo wa kiwango kikubwa cha
homoni hii huhusiana kwa karibu na ongezeko la mafuta mwilini.
4. Unajinyima usingizi wa kutosha
Kama wewe ni mmoja wa watu wale wanaokosa
muda wa kutosha kulala kwa ajili ya mihangaiko ya hapa na pale unapaswa
kuongeza muda wako wa kupumzika. Utafiti
uliofanywa kwa miaka 16 kwa wanawake 70,000 ulibaini wanawake waliolala masaa
matano au chini ya hapo walitarajiwa kuongezeka kilo 14 kuliko wale waliolala
masaa 7. Wataalamu hushauri watu wazima
kulala masaa 7 hadi 8 wakati wa usiku.
5. Una maradhi
Ikiwa kiwango chako cha homoni ya
Testosteroni kiko juu inaweza kuashiria kutokea kwa ugonjwa wa ovary (PCOS)
ugonjwa utakaosababisha iwe vigumu kupunguza uzito. “Ikiwa una umbo la tufaa na uzito uliozidi
kiasi, ni busara kumuona daktari” Dkt.
Kashyap anashauri, kwa maana hali
hiyo inaongeza hatari ya kupatwa na
ugonjwa wa kisukari
6. Mazoezi unayofanya hayatii changamoto za
kutosha katika mwili
Ili kuondoa kitambi cha muda mrefu ni
lazima kujidhatiti kwenye mazoezi magumu.
Utafiti uliochapishwa na jarida Medicine
and Science in Sports and Exercise, ulionyesha watu waliofanya mazoezi
magumu/mazito waliweza kupunguza kitambi haraka zaidi kuliko waliofanya mazoezi
mepesi. “Ikiwa lengo lako ni kuondoa
kitambi kabisa, basi huna budi kuchagua mazoezi kuondoa kitambi” asema Natalie
Jill, mtaalamu wa mazoezi kutoka San Diego.
7. Unakula mafuta yasiyohitajika mwilini
Mwili haumeng’enyi aina zote za mafuta kwa
njia ileile. Utafiti unaonyesha ulaji wa
vyakula vyenye mafuta kama nyama na maziwa huongeza mafuta tumboni na kufanya
kitambi. Wakati ulaji wa vyakula vya mafuta
kama parachichi, samaki na alizeti huweka mwili katika umbo zuri. Ingawa kula vyakula vyenye mafuta ya aina
yoyote hufanya mwili kuongeza uzito na kusababisha kitambi hivyo ni vizuri
kufurahia vyakula hivyo kwa kiasi kama jina la blogi yetu.
8. Unakula
sana vyakula vilivyosindikwa viwandani
Vyakula kama mkate mweupe, chipsi, vinywaji
vyenye sukari kama soda, juisi hufanya mwili kutanuka/kunenepa. Kitambi huambatana na kunenepa/kutanuka kwa
mwili, hivyo ulaji wa vyakula vya viwandani utarudisha nyuma jitihada/uwezo
wako wa kupambana na kitambi. Vyakula
vya asili kama matunda, mbogamboga na nafaka isiyokobolewa ambavyo ni vya asili
huufanya mwili kusinyaa na kusaidia kuzuia kitambi.
9. Hauna hamasa (motisha)
Ni kweli uko tayari kisawasawa kuondoa
kitambi? “kupunguza na kuondoa kitambi
kunahitaji ushirikiano wa vitu mbalimbali, vyakula vyenye kutia nguvu kidogo na
vyenye nyuzinyuzi kwa wingi pamoja na vyakula vyenye wanga na sukari kidogo
huku ukifanya mazoezi ya kupunguza uzito.”
Dk. Kashyap anasema. Ikiwa
umepania kupunguza/kuondoa kitambi unaweza kufanikiwa.
10. Una umbo la tufaa
“Ikiwa unene wako upo maeneo ya katikati na
maeneo ya hipsi (nyonga) na mapaja basi una umbo la tufaa (apple). Kwa muundo huu wa mwili ikiwa ni wa kurithi
basi kupunguza kitambi, itakuwa ngumu sana,” anasema Dk. Kashyap.
No comments:
Post a Comment