Watu wenye afya ya kisaikolojia hawajakamilika. Wana sehemu yao ya matatizo, dosari, na
makosa. Hata hivyo, ni jinsi
wanavyojitambua wenyewe na jinsi wanavyokabiliana na msongo na hali ya kushindwa kwao
ndivyo vinavyowatenganisha na watu wasio na afya ya kisaikolojia.
Watu wenye afya ya kisaikolojia wana sifa zifuatazo:
- Wanajikubali wenyewe na
wengine
- Wanajipenda
- Wanaonesha ipasavyo hisia
kamili za binadamu, chanya na hasi zote pamoja
- Wanatoa na kupokea msaada,
upendo na hali ya kujali
- Wanakubali maudhi
yanayotokea maishani
- Wanakubali makosa yao
- Wanaonesha uelewa na
kuwafikiria wengine
- Wanajitunza
- Wanawaamini wengine na
wenyewe pia
- Wanaanzisha malengo,
mafupi na ya muda mrefu
- Wanaweza kufanya kazi kwa
kujitegemea na kutegemeana na wengine
- Kuongoza mtindo wa maisha
ulioimarika wenye afya ambao unajumuisha mazoezi ya kawaida, lishe bora,
na usingizi wa kutosha.
Mfululizo wa Kawaida
wa Hisia
Unawajua watu ambao wanaonekana kuwa “juu” muda wote? Watu
hawa wanaonekana kuwa na ujasiri, furaha, na wamejawa na hisia nzuri masaa 24
ya wiki nzima. Japokuwa baadhi ya watu
wapo kama hivyo, kiukweli ni watu wa kipekee.
Kwa watu wengi, hisia ni zaidi kama zikiongezeka. Wakati mwingine wanajisikia vizuri kuhusu wao
wenyewe na wengine, mara nyingine hakuna kinachoonekana kwenda sawa. Hii ni ya kawaida na yenye afya. Maisha yana kupanda na kushuka, na wazo la
“mfululizo wa kawaida wa hisia” unaakisi haya mabadiliko.
Kujithamini
(self-esteem)
Kujithamini ni nini? Unajuaje pale mtu anapokosa
kujithamini? Watu wengi hujibu hili swali kwa kusema kwamba wanaelezea
kujithamini ambako ni chanya kama:
- Kujisikia ufahari
- Kuishi kwa kujiheshimu
- Kujichukulia mwenyewe
kwamba una thamani, ni wa muhimu, na mwenye kustahili
- Kujihisi vizuri kuhusu
wewe mwenyewe
- Kuwa mwenye kujiamini,
kujihakikishia
- Kujikubali mwenyewe
Watu wenye ngazi za chini ya kujithamini huwa wanaruhusu
wengine kuwatendea vibaya, hawajijali, na wana ugumu kuwa peke yao. Zaidi ya hayo, wana hali ndogo ya kujiamini
na kwa hiyo wanazuia kuthubutu na wanaamini kwa shida kama watu wengine
wanawajali. Watu wenye kiwango kidogo
cha kujiamini wanapenda kuchukulia vitu kibinafsi, muda mwingine wanaonekana
kama ni rahisi kuchukuliwa na fikra kupita kiasi na mtu asiyeridhika na
chochote mbali na anachofikiri kuwa ndicho, wanajikosoa wenyewe na wengine, na huamini
kwamba hawawezi kufanya chochote kwa usahihi.
Watu hawa huwa wana tabia ya kuona kuwa mambo yote ni mabaya juu ya
maisha, na wanajiona kana kwamba hawastahili kuwa na bahati nzuri.
Kujitegemea Kimawazo
Watu wenye kiwango kidogo cha kujithamini pia wana kiwango
kidogo cha kujitegemea kimawazo, kwa maana kwamba picha yao ya ndani, jinsi
gani wanajiona, ni mbaya sana. Kwa
sababu ya hiki kiwango kidogo cha kujitegemea kimawazo, watu wenye kiwango
kidogo cha kujithamini wana hatari zaidi ya kuwaruhusu wengine kuwatendea
vibaya au kuwatumia vibaya, na kushindwa kudai haki yao. Matatizo mengi ya kisaikolojia na nguzo zao
katika kiwango kidogo cha kujithamini, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kula,
matatizo ya madawa ya kulevya, huzuni, na ugonjwa wa wasiwasi.
Tunapata wapi kujithamini kwetu? Watu wengi watasema
wanapata kutoka kwa wazazi wao, waalimu, rika lao, ndugu, taasisi za kidini, na
vyombo vya habari. Wakati mambo haya kwa
hakika yanaweza kuathiri kujithamini kwetu kwa uzuri au kwa ubaya, yote ni mambo
ya nje. Kujithamini inashabihiana na
mtazamo binafsi wetu wa ndani. Kama
kujithamini kweli kunakuja kutoka mwonekano wetu wa nje, basi kuna haja ya
kubadili mazingira yetu na watu wanaotuzunguka.
Hii ndio sababu kwamba watu hupenda kujiambia, “Ikiwa ningetengeneza
hela zaidi, ningekuwa na gari zuri, ningekuwa nimeoa/nimeolewa, au ningekuwa na
kazi ya kifahari, ningejisikia vizuri sana.” Hii inaweza kuwa mzunguko wa
matatizo, kumuacha mtu muda wote akitafuta zaidi, na daima haridhiki. Hii pia inaweza kumsababishia mtu kuwa na
hali ya kutoridhika na chochote mbali na anachofikiri kuwa ndicho na
kutojikubali yeye mwenyewe.
Inakubalika kiujumla kwamba kujithamini huja kutoka ndani
mwetu na hatimaye ndani ya udhibiti wa kila mtu. Zaidi ya hayo, kujithamini haimo kwa wote au
hakuna ambaye hana kabisa, watu wengi wana viwango mbalimbali vya kujithamini,
kutegemea juu ya hatua zao za maendeleo, matukio kwenye maisha yao, na
mazingira yao.
Akili ya Kihisia
Kipengele cha tatu cha afya ya kisaikolojia ni kiwango cha
akili ya kihisia ulichonacho. Akili ya hisia
inahusu “uwezo wa kuwaelewa wengine na kutenda kwa busara kwenye mahusiano ya
binadamu.” Zaidi ya hapo, akili ya kihisia inaweza kugawanywa katika nyanja kuu 5:
·
Kujua
hisia zako. Hii inachukuliwa kuwa ni
msingi wa akili ya kihisia na inahusiana na kwa kiasi gani una hali ya kujitambua na
ufahamu ulio nao. Una haraka kiasi gani kuweza kutambua na kuzipachika hisia zako kwa jinsi unavyozihisi kuamua kiwango
chako cha akili ya kihisia.
·
Kusimamia
hisia zako. Ni kwa uzuri kiasi gani
unaweza kuonesha hisia zako ipasavyo na kukabiliana na hisia zako? watu wenye
shida ya kukabiliana na wasiwasi, dhiki, na kushindwa huwa wana viwango vidogo
vya akili ya kihisia.
·
Kujihamasisha
mwenyewe. Watu wanaoweza kujihamasisha
wenyewe huwa na kuwa wazalishaji wa hali ya juu zaidi na wako huru kuliko wale
wanaotegemea nguvu kutoka vyanzo vya nje kuwahamasisha. Jinsi unavyoweza kujihamasisha zaidi na
kushiriki katika shughuli zenye malengo, ndivyo unavyozidi kuikuza akili ya kihisia
yako.
·
Kutambua
hisia kwa wengine. Kipengele kingine
cha akili ya kihisia ni kiwango chako cha kutambua hisia za wengine ambacho unacho
au ni mwepesi kiasi gani kuhisi hisia za wengine na jinsi gani unajumuika na
watu wengine.
·
Utunzaji
mahusiano. Hii inahusiana na kiwango
chako cha stadi za kijamii. Kuwa na
ufanisi zaidi baina ya watu na kuweza kujadili mgogoro na kujenga mtandao wa
msaada kijamii, ndivyo unavyozidi kuwa na akili ya kihisia.
Bila
shaka, watu wana viwango tofauti vya akili ya kihisia na wanaweza kuwa na
kiwango cha juu katika Nyanja Fulani kuliko Nyanja nyingine. Watu wenye viwango vya juu vya akili ya
kihisia vya ujumla huwa wanapenda kuchukua majukumu ya uongozi, wanajiamini,
wana hali ya kudai haki zao, wanaonesha hisia zao moja kwa moja na ipasavyo,
wanajisikia vizuri, wanaomaliza muda wao, na hukabiliana vizuri na msongo.
No comments:
Post a Comment