Monday, September 19, 2016

AFYA YA KISAIKOLOJIA

afya ya kisaikolojia

Unajisikiaje kuhusu wewe? Wakati unapotumia rasilimali kutoka kwenye vipimo mbalimbali vya afya kwenye namna ambayo inakuruhusu kuelekeza ukuaji wako, kutathmini kwa undani maadili yaliyowekwa, kukabiliana kiufanisi na mabadiliko, na kuwa na mahusiano yanayoridhisha na watu  wengine, basi wewe una afya kisaikolojia.  Utafiti katika eneo la afya ya saikolojia umeonesha kwamba kuna muunganiko kati ya akili na mwili ambako mambo ya kijamii, kibaiolojia na kisaikolojia huingiliana kushawishi afya au ugonjwa. 
Tunajua kwamba hali yako ya kisaikolojia ina athari kubwa katika afya ya kimwili: msongo, huzuni, na wasiwasi vimekuwa vikihusishwa na jinsi mfumo wako wa kinga unavyoitikia na inaweza kutatiza afya ya kimwili.  Tafiti zimeonesha kwamba wagonjwa mahututi wa saratani ambao walikuwa wana afya nzuri ya kisaikolojia waliishi maisha marefu.

Afya ya kisaikolojia imekuwa ikihusishwa pia na kuendeleza na kudumisha kujithamini, kujitegemea kimawazo, na kiwango cha juu cha akili ya kihisia.  Afya ya kisaikolojia ni zaidi ya kukosekana kwa ugonjwa wa akili.
Share:

No comments:

Post a Comment