Licha
ya juhudi zao nzuri ya kuwa chanya na imara, watu wengi wana kiwango kidogo
kuliko kile kiwango cha chini cha afya ya kisaikolojia. Kuna baadhi ya mijadala kuhusu ni kwa kiasi
gani watu wanatawala afya ya kisaikolojia.
Makubaliano ya jumla ni kwamba mambo mawili, asili na malezi, yanaathiri
afya ya kisaikolojia, lakini kuna maoni tofauti juu ya kiasi gani kila moja
inachangia katika ukuaji wetu wa kisaikolojia.
Asili inahusu mambo ya asili tuliyozaliwa nayo pamoja na vile vinasaba
ndivyo vinavyoamua kiwango chetu cha afya ya kisaikolojia. Malezi ni athari ambayo mazingira, watu, na
mambo ya nje yanayo juu ya afya yetu ya kisaokolojia.
Wote tunawajua baadhi ya watu ambao
wanachachawika sana au wana wasiwasi kwa asili, na wengine ambao ni wachangamfu
kwa asili. Tunaonekana tukizaliwa na
mtazamo kuelekea kwenye afya fulani ya kisaikolojia, ambayo mara nyingi
inafanana na wazazi wetu. “Yuko makini
kama baba yake” au “Anachekesha kama mama yake” ni maneno watu wanayoweza
kudokeza kuhusu muunganiko huu wa vinasaba.
Mambo ya kimazingira kama vile mahusiano ya kijamii, maelewano ya
familia, rasilimali fedha, kazi na mawazo ya kitaaluma, hali zinazoleta msongo
au matukio na hata hali ya hewa inaweza kuathiri kiwango chako cha
kisaikolojia.
Wednesday, October 5, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment