Kuzaliwa kwa mtoto ni moja ya miujiza mikuu ya Mungu ya
uumbaji. Mtoto mchanga aliyezaliwa miezi
yake kamili anakuwa na uzito kati ya kilo 2.5 mpaka 4.6 (ratili 5 – 10) ikiwa
ni uzito wa wastani kilo 3.4. urefu kwa
kawaida ni sm 45 mpaka 55 (inchi 18 – 22) ikiwa ni wastani wa sm 50 (inchi
20). Mzingo wa kichwa ni kutoka 32.6
mpaka 37.2, ikiwa ni wastani wa sm 35 (inchi 14).
Uwiano wa mwili wa mtoto wanapozaliwa upo tofauti kutoka
watoto wadogo wachanga, watoto na watu wazima.
Kichwa kwa kawaida ni kikubwa, uso ni wa mviringo zaidi, taya dogo zaidi
kuliko watoto wakubwa na watu wazima.
Kifua kinaonekana kuwa mviringo kuliko kuwa bapa, na tumbo kwa kawaida linajitokeza na mikono na miguu ni mifupi.
Mtoto yuko tayari kula dakika chache baada ya kuzaliwa na
anaweza kunyonyeshwa maziwa ya mama mapema, dakika 30 baada ya kuzaliwa. Mwanzoni mtoto mchanga anadhihirisha njaa kwa
muda tofauti tofauti, lakini mwishoni mwa juma la kwanza la maisha inaanza kuwa
wa kawaida kati ya saa 2 na 5. Yapasa
mtoto aruhusiwe kunyonya anapohitaji.
Haja kubwa ya kwanza inatoka ndani ya saa 24. Ni kijani kibichi kinachoitwa
“meconium”. Hiki kinabadilika rangi
mpaka siku ya 7 kinakuwa cha njano.
Watoto wachanga hutoa haja kubwa mara 3 – 7 kwa siku. Wengine wanatoa haja kubwa kwa muda pungufu
kuliko kawaida na anaweza kuchukua siku 3 – 4 bila kupata choo. Ikiwa watoto wachanga hao wananyonya maziwa
ya mama tu, kupata choo kwa muda tofauti tofauti hakuna tatizo lo lote.
Kutoka muda wa kuzaliwa mtoto mchanga anauwezo wa kuona vitu
na anaweza kufuatilia mjongeo wa vitu hivi.
Wanapendelea vitu vinavyofanana na uso wa mwanadamu. Watoto wachanga wanapendelea sauti za juu au
sauti za kike, na mwishoni mwa juma la kwanza la maisha, wanaweza kugeuza
vichwa vyao kwa urahisi zaidi kuelekea inakotokea sauti za mama zao.
Maziwa ya mama yanatosha kumlisha mtoto katika miezi sita ya
kwanza ya maisha ya mtoto. Kwa watoto
ambao hawanyonyeshwi maziwa ya mama bado inapendekezwa kuwa wanyonye maziwa kwa
miezi sita ya kwanza ya maisha yao.
Baada ya miezi sita chakula cha nyongeza kinaweza kutumika. Hivi vinajumuisha lishe kamili ya vyakula vya
wanga (mfano chakula cha mchele, viazi na mahindi) jamii ya kunde (maharage,
choroko, njegere, mayai nk). Matunda
nayo wapewe kwa namna ambayo wanaweza kumeza.
Inashauriwa kuwa kunyonyesha maziwa ya mama kuendelee kwa muda
usiopungua miaka miwili (kama mama ana afya nzuri).
Watoto wachanga kwa kawaida wanapoteza asilimia 10 ya uzito
wa kuzaliwa katika juma lao la kwanza la maisha, lakini wanaupata tena baada ya
kufikia umri wa siku 10. Mtoto mchanga aliyezaliwa
miezi kamili kwa kawaida uzito wake unakuwa maradufu ya uzito wa kuzaliwa
anapofikisha umri wa miezi 5, na unakuwa mara tatu akiwa na mwaka mmoja. Urefu wa watoto wachanga wa kawaida
unaongezeka katika mwaka wa kwanza kwa sm 25 – 30 (10 – 12). Utosi waweza kuongezeka ukubwa baada ya
kuzaliwa, lakini unaanza kuwa mdogo na kufunga kati ya miezi tisa na kumi na
nane ya umri wake. Na sehemu ya nyuma ya
utosi inafunga baada ya miezi minne ya umri wa mtoto mchanga.
Meno ya kwanza ya mtoto mchanga yanaanza kati ya miezi
mitano na tisa. Kwa muda wa miezi tisa
watoto wachanga wengi wanayo meno 6 – 8.
Kwa nadra mtoto anaweza akawa na meno mawili baada ya mwaka mmoja bila
ya kuwa na ushahidi wowote wa shida katika ukuaji wake.
Matukio Muhimu
Hii inaelekeza kwenye maendeleo ya ukuaji wa uwezo wa misuli
ya mwendo.
Udhibiti wa kichwa yaani uwezo wa mtoto kukiweka kichwa chake katika nafasi ya kusimama wakati anaposhikwa au akiwa katika nafasi ya kukaa, unafikiwa karibu baada ya miezi 3 ya umri wake. Mtoto ana uwezo wa kurejesha tabasamu la uso unao tabasamu kwa majuma 3 mpaka 5 ya maisha yake. Kwa miezi 5 – 6 mtoto ana uwezo wa kubiringika. Pia ana uwezo wa kuokoa vitu vilivyo jirani na kuvihamisha kutoka mkono mmoja kwenda mwingine na mdomoni. Mtoto mchanga anajifunza kukaa akiwa na miezi 6 – 7 na kutambaa miezi 9 – 10.
Mtoto mchanga anaanza kusimama kati ya miezi 10 – 12 na
kutembea mara baada ya hapo. Watoto
wachanga wengi wana uwezo wa kukimbia wakiwa na umri wa miezi 18.
Uwezo wa kusema unakua kutoka karibu miezi 15 wakati mtoto
anapoanza kutamka silabi moja moja ya maneno au majina ambayo yanazungumzwa
sana.
Watoto ambao wamezaliwa njiti wana mfumo wa ukuaji taratibu
na wanaweza wakapatwa na maradhi kama kupungukiwa damu na matege.
Wanachoweza Kufanya
Wazazi
Wazazi/walezi wanaweza kufanya mengi ili kuhakikisha kuwa
wanawasaidia watoto wao kukua na kuongezeka kwa kawaida. Ni muhimu kwa wazazi kujua namna watoto
wanavyokua kimwili, kiakili, kihisia, kijamii na kiroho. Kwa njia hii watakuwa na uwezo wa kuwapa
watoto wao mahitaji ya haraka, kuwapa shughuli
sahihi za michezo ili kusisimua uwezo wa kujifunza na utayari wa maisha
yake ya baadaye. Kiambato muhimu sana
katika utunzaji wa makini wa upendo, uchangamfu wa mtu mzima.
Ukuaji Kiroho
Mpeleke mtoto wako katika program ya kanisani
iliyoandaliwa kwa watu wa umri wake.
Kama kanisa lenu halina program hiyo, ianzishe. Wazazi wengine wanaweza kujiunga katika
maandalizi na wakati wa kufundisha. Uwe
na muda maalum wa ibada nyumbani. Muda
huu wa maalumu utaisaidia familia iwe na muda maalumu wa kujifunza biblia kwa
pamoja. Biblia inafundisha juu mtazamo
wa mtu katika ujumla wake, ikijumuisha akili, mwili na kiroho na kijamii. Na inazungumzia juu ya maendeleo ya Yesu
kuwa: “yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo akimpendeza Mungu na wanadamu.”
(Lk 2:52) Tuombe hekima kutoka juu ili tufuate kielelezo cha maisha ya Yesu.
No comments:
Post a Comment