1.
Je, Ninayo Maambukizo Yatokanayo na Ngono?
Ni muhimu kwa mwanajinakolojia kufutilia mbali kitabibu kuwa huna
maambukizi yaletwayo na ngono. Kama
ikibidi vipimo zaidi kuondoa “Chlamydia” Kaswende, Kisonono na virusi viletavyo
UKIMWI lazima vichukuliwe kama ikithibitika kuwa yako maambukizi yatokanayo na
ngono, tiba lazima imjumuishe mwenzi wako ili kuzuia maambukizi yasitokee
tena. Uchunguzi wa kila mwaka wa
mwanajinakolojia, kwa wanawake unawapa fursa nzuri kubainisha hali zai dhidi ya
virusi viletavyo UKIMWI.
2.
Je, Njia Ninayotumia Kuzuia Mimba Ndiyo Inayonifaa Zaidi?
Utakapomtembelea mwanajinakolojia njia za kuzuia mimba
zitachunguzwa. Baadhi ya wanawake
wanapata madhara kwa kutumia njia hizi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzito,
kwa njia za kuzuia mimba kwa kutumia homoni, hedhi inayozidi na wakati mwingine
inatoka kwa vipindi tofauti, kupoteza ashiki na kutohusika na utumiaji wa kila
siku wa kidonge. Kweli, ni vigumu
kutabiri mwitikio wa mtu kwa aina Fulani ya njia ya kuzuia mimba. Pamoja na hayo ni muhimu kujadili chaguzi
zingine zilizopo na ikiwezekana badilisha aina hiyo ikibidi. Kwa wale ambao wamefikia idadi ya familia
wanayohitaji, njia za kudumu za kufunga Mirija ya Mke (BTL) au kumhasi mwanaume
inaweza kufikiriwa.
3.
Je, Maambukizi ya Mfumo wa Haja Ndogo Yaani UTI ni Kitu Gani?
UTI ni maambukizi yoyote ya mrija wa kupitisha haja ndogo na kibofu
(sehemu ya chini ya mfumo wa haja ndogo) au mfereji wa ureta na figo (sehemu ya
juu ya mfumo wa haja ndogo) kwa urahisi ni maambukizo yoyote katika mfumo wa
kutengeneza au kutoa haja ndogo mwilini.
Mfumo huu kwa kawaida ni safi kabisa yaani haujatekwa na bacteria au
kiini cha maradhi. Mambo mawili kwa
kawaida yanasabisha mwanamke ashambuliwe kwa urahisi na UTI:
1)
Mrija wa kupitishia haja ndogo nje kwenye uke ni
mfupi kwa hiyo uchafuzi wowote wa bacteria unaweza ukapata urahisi kufika
kwenye kibofu.
2)
Mlango wa mrija wa kupitishia haja ndogo upo
karibu na Uke na mlango wa haja kubwa.
Kumbuka kuwa mshipa wa kupitishia haja ndogo ni safi kabisa lakini
milango wa uke na mlango wa haja kubwa
haviko safi kabisa kwa sababu vinaficha mamilioni ya bacteria. Hivyo uchafuzi wa mrija wa kupitishia haja
ndogo unafanyika kirahisi. Dalili za UTI
zinajumuisha kwenda haja ndogo mara kwa mara tena inayoambatana na
maumivu. Katika hali mbaya sana wakati
maambukizi yamefikia sehemu ya juu ya mfumo wa haja ndogo homa, kutetemeka, na
maumivu kwenye ubavu vinaweza vikajionesha kwa wazi. UTI si maambukizi yanatokana na ngono. Pamoja na hayo inaweza kuboreshewa mazingira
na tendo la ngono kwa sababu ya ongezeko la uwezekano wa kudhuru sehemu
inayolinda mrija wa kupitisha mkojo usichafuliwe.
4.
Je, Hedhi Yangu ni
ya Kawaida?
Mpangalio wa kutoka damu unatofautiana kulingana na mtu mmoja mmoja. Lakini muda unapaswa kuwa siku mbili mpaka
siku saba. Kipindi kati ya hedhi na
hedhi kiwe kati ya siku 21 na 35. Muda
huu ni kipindi kutoka siku ya kwanza ambayo hedhi inatokea mpaka kwenye siku ya
kwanza kwa hedhi inayofuata. Damu
inatakiwa iwe nyeusi kwa rangi na haitakiwi kuganda. Wanawake wengi wana vipindi vya kawaida vya
hedhi yao. Tofauti yoyote kutoka katika
mpangilio huu wa kawaida unahitaji uchunguzi na mwanajinakolojia.
5.
Nifanye Nini na Upotevu wa Ashiki?
Wanawake wengi hawako tayari kueleza uzoefu wa matatizo yao ya
kingono. Mengi ya matatizo haya yanaweza
yakatatuliwa na mwanajinakolojia.
Kisababishi kikubwa cha ashiki ndogo kwa wanawake vijana ni madawa, hasa
hasa yanayoongeza nguvu na vidonge vya kuzuia hofu. Wanawake wengine wanaeleza juu ya kupungua
kwa ashiki kutokana na aina ya njia wanayotumia kuzuia mimba. Muunganiko wa vidonge vya kumeza kuzuia
mimba, homoni ya kike inayoweza kuingizwa kwa sindano au kupandikiza. Usumbufu au maumivu wakati wa ngono yanaweza
kusababisha matatizo ya ngono na sababu kuu inaweza ikawa kutoka matatizo
makubwa ya kiutabibu kama maradhi ya uvimbe kwenye mfuko wa uzazi, kuvimba kwa
mfupa wa nyonga kwa hali rahisi. Kama
uchachu wa uke na kubadilika badilika kwa ute wa uke.
Mwanajinakolojia wako anaweza akaanzisha njia
za kukupeleka kwa mtaalamu wa tiba ya ngono.
6.
Je, Historia ya Unyanyasaji Kingono au Vinginevyo Ina Madhara Kwenye Afya ya Uzazi Wangu?
Unyanyasaji wa ngono katika watoto na vijana wakubwa inaendelea kutokea
katika nchi ya Kenya na nchi zingine.
Utafiti unaonesha kwa ndugu wa karibu huwa ndio wahusika wa makosa haya;
Yanaweza kuwepo makovu ya kudumu ya kimwili kutokana na matukio haya lakini mengi
zaidi ni yale yaliyo matokeo ya kisaikolojia yaliyijificha na ambayo yanaweza
yakajionesha yenyewe baadaye kama magonjwa ya kimwili. Mtendewa anaelekea kushikilia wasi wasi na
mfadhaiko juu ya jambo hilo, halafu anakuza dalili za kimwili mara nyingi maumivu
kwenye fupa la nyonga ambayo inaaksi maumivu ya kiakili; kutaja kiwewe cha
ngono ya huko nyuma linaweza kuwa la msaada sana kwa mwanajinakolojia kutambua
wa ugonjwa huo. Kama hakuna kinachotajwa
mwanamke anaweza akapitia vipimo vingi vikionesha matokeo ya kawaida. Lakini kama tabibu anajua juu ya mashambulizi
ya huko nyuma anaweza kumshauri mhusika moja kwa moja au kumpeleka kwa mtaalamu
wa magonjwa ya mawazo na wakati huo huo kuzuia vipimo vingine kuchukuliwa.
7.
Je, Uvutaji Sigara
na Utumiaji Kilevi Unaathiri Afya ya Uzazi Wangu?
Uvutaji sigara ni jambo hatarishi kwa kusababisha saratani kwa wanaume na
wanawake. Uvutaji wakati wa ujauzito
husababisha kujifungua kabla ya wakati, kujifungua mtoto mwenye uzito wa chini,
na kupasuka kwa utando kabla ya wakati wake; kuharibika mimba na hata kifo papo
hapo baada ya kuzaliwa mtoto. Matumizi
ya vidonge vya kuzuia mimba na uvutaji
vinaongeza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi. Wanawake ambao wanavuta na kuchelewesha kuzaa
mtoto wanajiweka mahali pa hatari kwa ugumba baadaye zaidi kuliko wale ambao
hawavuti. Wanawake wanaovuta
wana uwezekano wa kukatika hedhi mapema zaidi ya wale ambao hawavuti. Unywaji kilevi kwa wingi unavuruga ukuaji na
maendeleo wakati wa kubalehe. Inavuruga
mzunguko wa hedhi na utendaji wa via vya uzazi.
Unywaji wa kilevi unaweza ukasababisha ugumba na uharibikaji mimba wa
mara moja na pia ukuaji usio wa kawaida wa mtoto na maendeleo yake.
8.
Ni Mara Ngapi Lazima Nifanye Nipime Saratani ya Shingo ya Kizazi?
Saratani ya shingo ya uzazi ni ya pili katika kusababisha vifo vya akina
mama baada ya saratani ya matiti. Lakini
inaweza ikazuiliwa kwa kutambua na kutibu mapema kabla ya kujitokeza vitu
visivyo vya kawaida vya saratani. Kwa
kawaida wanawake wote walio katika kundi la uzaaji na ambao wamepata uzoefu wa
ngono lazima wapime kila mwaka. Lakini
kama kipimo kimefanyika miaka mitatu mfululizo na hali iko kama kawaida basi
inaweza ikarudiwa ndani ya miaka mitatu baada ya pale. Ni wanawake tu ambao wameondoa mji wa uzazi,
kwa sababu ambazo hazihusiani na saratani ya shingo ya uzazi, ndio hawana haja
ya kupima.
9.
Ni Kitu Gani Kinachosababisha Saratani ya Shingo ya Uzazi na Je Kuna Chanjo ya Kuizuia?
Sasa inafahamika kuwa saratani ya shingo ya uzazi kwa kawaida
inasababishwa na “Human Papilloma Virus” (HPV) kirusi cha uvimbe wa mwanadamu. HPV ni kirusi cha kawaida. Katika aina nyingi na mbalimbali za HPV
baadhi hazina madhara na nyingine zinaweza kusababisha maradhi ya viungo vya
uzazi. Wakati watu wengi wanakisafisha
kirusi wale ambao hawafanyi hivyo wanaweza wakapata saratani ya shingo ya
uzazi, vidonda kabla ya saratani, na sugu kwenye viungo vya uzazi. Hivi karibuni chanjo yenye uwezo wa kuzuia
saratani ya shingo ya uzazi kwa kuzuia maambukizi ya HPV zimeshaanzishwa. Moja ya chanjo hiyo inayoitwa “GARDASILTM”
(aina za 6, 11, 16, 18). Mchanganyiko wa
chanjo uliokuzwa na MSD nyingine inayoitwa “CERVARIXTM” (HPV 16 na 18) zilizo
kuzwa na GSK. Zipo aina zaidi za mia
moja ya virusi hivi vya HPV. Chanjo za
HPV hazitakinga dhidi ya aina zote isipokuwa aina ya 6, 11, 16 na 18 zimechaguliwa
kwa sababu zinasababisha zaidi ya asilimia 70 ya saratani ya shingo ya uzazi na
asilimia 90 ya sugu kwenye viungo vya uzazi ulimwenguni kote. Chanjo inaweza isimlinde kwa ukamilifu kila
mmoja anayeipata na hivyo ni muhimu kuendelea na vipimo vya saratani ya shingo
ya kizazi.
10.
Ni Mara Ngapi Ninapaswa Kufanyiwa Uchunguzi wa Matiti?
Uchunguzi wa matiti ni muhimu katika kutambua
uvimbe ambao unaweza ukawa saratani.
Saratani ya matiti ndio sababu inayoongoza kwenye vifo vya wanawake
ulimwenguni kote. Inabidi kila mmoja
afanye uchunguzi binafsi wa matiti angalau mara moja kwa kila miezi
mitatu. Kwa nyongeza, lazima uwe na
uchunguzi wa matiti ambao unafanywa na daktari mara moja kwa mwaka. Hii ni lazima ili kutambua utofauti wowote
ambao haukutambuliwa na mtu binafsi.
Inapendekezwa kuwa wanawake wenye zaidi ya miaka 40 lazima wafanyiwe
uchunguzi wa matiti kwa kutumia eksirei kila mwaka.
No comments:
Post a Comment