Nyumba ya kikristo ni mahali pa muhimu sana ambapo
tunakamilishana kila mmoja na mwenzake.
Ni katika hali hii kwamba wanafunzi wawili wa Biblia ambao wanafahamika
sana walisema wakati Fulani kuwa nyumbani hapakukusudiwa kuwa mahali ambapo mtu
anakamilika kama mtu. Mtu anamhitaji
mwingine ili kuwa kamili.
Kwa nyumbani kukamilisha kitu cha thamani kuu kama hiki
kunahitaji kuwa mahala salama kwa sababu kumetengwa kuwa sehemu salama kukuza
maadili kwa nyumba ya kikristo yenye afya.
Kamusi ya kiingereza ya Collins iliyo chapishwa mwaka 2003
inalifasili neno maadili kama hali ya kuwa na shauku ya kitu mara nyingi
kuhusiana na rasilimali kama vile matumizi yake au ubadilishano: kufaa, stahili
au umuhimu sahihi. Kwa namna nyingine
maadili yanaweza yakafasiliwa kama kanuni ya maadili na imani au kipimo kilicho
kubalika cha mtu au kikundi cha kijamii.
Hivyo, maadili yametolewa au yameanzishwa yawe pale ili yaweze kusaidia kujenga maisha
ya Kikristo, ya kifamilia, na ya kinyumba.
Biblia katika kitabu cha Mwanzo 2:18 inathibitisha kuwa
inachukua wawili kumfanya mmoja. Bwana
akasema “Si vema mtu awe peke yake---” kwa hiyo upweke haukuwa katika mpango wa
Mungu kwa afya ya maisha yetu ya kifamilia.
Swali ambalo mtu anaweza akajiuliza mwenyewe ni hili kwa nini wawili na
sio watatu?
Maisha ya mume na mke ni klabu maalumu kwa ajili yao wawili
tu. Ni mchezo au mpango wa watu wawili,
hivyo kuacha nje wengine wote.
Wakristo wote wenye shauku ya kuwa na nyumba bora ya
kikristo lazima watambue kuwa katika macho ya ulimwengu thamani ya mtu inapimwa
kwa, “thamani ya mali aliyo nayo? Lakini vitabu vya mbinguni vinaandika thamani
yake kwa uwiano wa mema aliyo nayo? Lakini vitabu vya mbinguni vinaandika
thamani yake kwa uwiano wa mema aliyoyakamilisha kwa kutumia mali
alizokabidhiwa. [E.G. White 2 Selected Message Vol.2, 193]
Jambo la msingi katika “wawili kuwa mmoja”, ni kwamba watu wawili
lazima wawe kamili wao wenyewe. Watu
wawili hawa wanahitaji kuwa watu wazima.
Ni kwa namna gani wanaweza kuwa watu wazima? Mtu anaweza kuwa mtu mzima
kwa kuweza kuwajibika, kwa kutawala hisia, mwelekeo, tabia, uchaguzi, na mipaka
yake. Mtu aweza pia kuthibitisha kuwa mtu
mzima kwa kutawala shauku, talanta na upendo wake.
Maadili Sita ya Msingi kwa Nyumba Bora ya Kikristo
Katika maisha ya leo tunatambua kuwa ipo haja kwa nyumba za
Kikristo kuwa bora zaidi. Ni kwa sababu
wakati tunazo nyumba bora za Kikristo ni wazi tutakuwa wanafamilia bora na kama
tuna wanafamilia bora kwa hakika tutakuwa na wakristo bora. Kama tunao wakristo bora itakuwa wazi zaidi
kuwa watu wengi watafaulu kuingia mbinguni.
Kwa hiyo yako maadili ambayo tunahitaji kuyajenga kama
tunataka kuwa na nyumba bora za kikristo.
Tunahitaji kufikiri kwa upana na kuona picha kubwa ya maisha na nyumba
zetu. Hivyo kila mkristo anahitaji
kujenga maadili yafuatayo:
1. Utamaduni wa Upendo wa Yehova
Kama mtu ana shauku ya kupata juisi ya
maembe ni wazi anahitaji kupanda miti ya maembe. Kama anataka kupata juisi ya malimau lazima
apande mti wa mlimao. Hawezi kutegemea
kupata juisi ya limao wakati anapanda miti ya miparachichi. Haiwezekani kabisa!
Kwa utamaduni wa kumpenda Mungu ni maadili
namba moja katika maisha ya mkristo.
Usitegemee kumpenda mtu yeyote kama humpendi Mungu. Hata hivyo, ulimwengu unaweza kutuona
kirahisi kama tuna upendo wa Mungu. Kama
ilivyothibitishwa katika Yohana 5:42 “lakini nawafahamu ninyi hamna upendo wa
Mungu ndani yenu”.
Somo
la kwanza: kulingana na uzoefu wangu
katika huduma ya ushauri nasaha tatizo kubwa ambalo familia inapata ni matokeo
ya wanafamilia kusahau kumpa Mungu nafasi yake katika maisha yao na katika
nyumba zao.
2.
Utamaduni
wa upendo wa mwenzi wako
Mwenzi kwa ujumla amefasiliwa kuwa ni mbia
wa mtu katika ndoa [Collins English Dictionary 2003]. Hivyo kabla hujajipenda mwenyewe unahitaji
kwa kweli kumpenda mwenzi wako. Hapa
Biblia inatuambia kuwa tunahitaji kufuata mfano wa Yesu, ambaye ana utukufu
wote mbinguni, lakini akaamua kushuka chini kwenye nafasi ya chini kuliko
nafasi zote kama ilivyosemwa na Maxwell JN .
anaiita hii kuwa ni sheria ya kujitoa kwa hali ya juu. [Fil 2:3-4] Kwa hiyo tunahitaji kufikiria mahitaji
ya wenzi wetu kabla ya mahitaji yetu.
Katika maisha ya wanandoa upendo lazima uwe
kitu namba moja katika yote watakayofanya iwe kwa siri au hadharani. Wakati hili litakapoheshimiwa utukufu na
heshima atapewa Bwana.
Somo
la pili: kwa ufahamu wangu familia
yoyote inayohitaji kuwa na maisha bora, kila mwanafamilia lazima kwanza
afikirie mambo yaw engine, au kuchukua mambo ya mwenzi wake kwanza.
3. Utamaduni wa Ukweli/unyofu
Watu wengi katika jamii wamepoteza fikra ya
unyofu. Kamusi ya Collins, ya 2003, linafasili
neon unyofu kama kuwa ni hali ya kuwa mkweli.
Unyofu unamaanisha kutokuwa na mwelekeo au tabia ya kudanganya, kusema
uongo, kuiba au kutokuwa mkweli.
Familia nyingi ziko chini ya mvuto wa roho
ya uovu na kama hii ndivyo ilivyo si rahisi kwa ukweli kuonyeshwa katika yote
wanayopanga na kufanya. Lakini pamoja na
hayo Roho Mtakatifu kwa hakika ataijaza familia inayofundisha wanafamilia wake
kuwa wakweli na hivyo kubadilisha maisha yao.
E.G. White anatushauri kuwa “hebu tabia yenu ifunue kiwango cha juu
ambacho wote wanaweza kukifikia”.
[Ministry of Healing 198].
Anaendelea kutuambia kuwa katika ulimwengu
huu waume na wanawake bado hawajaanza kuelewa makusudi ya kweli ya maisha. Labda hii ni kwa sababu tumepoteza umaana wa
unyofu katika maisha yetu na katika maisha ya familia. Wakati tunaishi katika aina hiyo ya maisha,
shetani anafurahi kwa sababu ni kusudi lake kutuona sisi hatuingii mbinguni ili
kudhihirisha kuwa Mungu ni mbaya.
Sasa wale wote ambao tumekwisha
kufahamishwa tunahitaji kwa kweli kuimarisha utamaduni wa kweli katika familia
zetu.
Somo
la tatu: uzoefu wangu katika huduma
ya ushauri nasaha ni kwamba matatizo mengi ambayo hayajatatuliwa katika familia
yanasababishwa mara nyingi na wanafamilia ambao hawafuati sheria ya uaminifu –
Kwa hiyo mwanafamilia yeyote ambaye anataka kuwa na familia bora ya kikristo
anahitajika kuwa mwaminifu. Uaminifu
katika mambo makubwa na madogo.
4. Utamaduni wa uaminifu
Je inamaanisha nini kuwa mwanimifu? Ni hali
ya mtu ambaye ni mwaminifu. Wakati mtu
anapokuwa mwaminifu imesemwa kuwa, mtu Yule ana imani, anabaki kuwa mkweli,
mwenye msimamo, na mtiifu.
Katika suala la maisha ya wenzi uaminifu
utaamsha shauku ya maisha bora sio kwa mmoja bali kwa wote.
Katika maisha ya leo shetani anafurahi sana
wakati mmoja wa wanandoa anapokuwa si mwaminifu. Kwa sababu anafahamu kabisa kuwa hili
litadhoofisha wanandoa na familia. Hivyo
wengi hawataingia mbinguni. Uaminifu ni
moja ya masharti ya maisha bora katika familia kwa wanandoa kuthaminiwa. Ili kuwe na mafanikio katika maisha ya
wanandoa, wabia hawa lazima wawe na umoja.
Hebu tuthaminiane kwa kuwa waaminifu.
Hivyo E.G. White anapendekeza kwetu kuwa “Thamani ya mwanaume au
mwanamke kama Mungu anavyomkadiria ni
katika muungano wake na Kristo [OHC 149]” Wakati tumeungana tunafanikiwa.
Somo
la nne: washauri wanaamini kuwa
wanafamilia ambao wameamua au wamechagua kuishi maisha yasiyo ya uaminifu
wanazalisha matatizo mengi katika familia.
Kwa hiyo mwanafamilia yeyote anaye tegemea maisha bora ya kifamilia
anahitajika kuwa mwaminifu.
5. Utamaduni wa huruma na msamaha
Utafiti wa neno huruma katika Biblia
unaonesha kuwa neno huruma kwa kawaida linatumika kama sifa ya kiuungu na
kibinadamu [New Bible Dictionary 1196].
Neno huruma linaweza kumaanisha hisia anazozipata mtu wakati ameguswa na
mateso yaw engine, na tendo la kuingia ndani ya mateso yaw engine kwa makusudi
ya kuyaondoa [New Dictionary of Christian Ethics and Pastoral Theology 2003].complete
dictionary for home school and office chapisho la mwaka 1977 inafasili kuwa
huruma ni kusikitishwa au kuwa na moyo wa huruma kwa mateso na mikasa ya
wengine na kuwa na shauku ya kuwapa msaada au kuwaonyesha huruma.
Kwa upande mwingine, msamaha kwa ujumla
unachukuliwa kuwa ni utambuzi kwamba toba ama ya mmoja au ya wote ni ya kweli
na kwamba uhusiano mwema umerejeshwa au umepatikana [New Dictionary of
Christian Ethics and Patoral Theology 2003].
Msamaha ni vyote tendo la kusamehe na hali ya kusamehewa [ The
Complete Dictionary for Home School and Office1977].
Maisha katika familia pasipo huruma na
msamaha hayawezekani. Nyumba bora ya
kikristo inahitaji kujifunza roho ya huruma na msamaha. Hii ndiyo thamani ambayo kila mmoja wetu kama
mshiriki wa familia na wa nyumba lazima tusidhoofishe. Nyumba nyingi za kikristo ziko mbali sana na
kukamilisha hili.
Somo
la tano: kwa upande mmoja tunakuza
tendo la kuwa na moyo wa huruma, na unaosamehe, na kwa upande mwingine tunakuza
hali ya kusamehewa. Yote mawili lazima
yaende pamoja katika nyumba bora ya Kikristo.
6. Utamaduni wa utakatifu
Kamusi ya New Dictionary of Christian
Ethics and Pastoral Theology 1995, inafasili utakatifu kama kustahimili katika
suala la ukweli na udanganyifu. Wakati
tunapoitazama Collins English Dictionary 2003 inaafiki kuwa utakatifu ni hali
ya kuwa mtakatifu.
Kujifunza biblia kunaonesha kuwa utakatifu
ni neno ambalo ni la kidini kabisa na ni sifa ya msingi ya Mungu. [The New Dictionary of Christian Ethics and
Pastoral Theology 1995].
Kila mwanafamilia lazima atambue kuwa tabia
hii lazima ijengwe. Ni katika hali hii
Paul anasema kwamba, “Au hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho
Mtakatifu ambaye anakaa ndani yenu, mliyepewa na Mungu, na ninyi si mali yenu
wenyewe?”
Ni kwa bahati mbaya kwamba washiriki wengi
wa familia za kikristo wamechagua kuongoza chombo baharini kinyume na upande
ule ambao Biblia inapendekeza katika maandishi ya Paulo. Uchunguzi unaonesha kuwa matatizo mengi katika familia yanatokea kwa sababu washiriki
kwa makusudi kabisa wameamua kutozingati sifa hii ya Mungu. Wanawaleta katika nyumba ya familia ya
kikristo, marafiki, ndugu wa kiume wazazi na wengi wengine ambao hawataweza
kuwasaidia kutafuta ufumbuzi wa hoja hizo bali watayafanya yawe mabaya zaidi.
Washiriki wote wa familia bora ya Kikristo
lazima wajione wenyewe kuwa ni watakatifu na wametengwa kwa kila mmoja ajili ya
mwenzake.
Hitimisho
Nyumba nyingi za kikristo hazina afya. Hivyo haziwezi kuitwa nyumba bora za
kikristo. Kwa hiyo ipo haja ya kufanya
matengenezo katika njia zetu za kuishi, kwa kuchagua mwenzi sahihi, kufunga
milango ya nyumba zetu bora za kikristo, kuzifanya nyumba zetu za kikristo ziwe
duara la ndani, kuwaacha wengine wote nje ya klabu, kwa sababu katika hali
nyingi wa nje wanaathiri wa ndani.
No comments:
Post a Comment