Tumbaku ni kitu ambacho kimekubalika kijamii ulimwenguni
kote. Matumizi yake yameenea katika
jamii zote na makundi yote ya kijamii, wanaume na wanawake, matajiri na
maskini, wadogo na wakubwa, vijana na wazee, isipokuwa tu kwa watoto wadogo
sana. Uzalishaji na utengenezaji wake ni
shughuli ya kiuchumi ya mabilioni ya pesa, ikiajiri mamilioni ya wafanyakazi na
kulipa kodi ya mabilioni kwa serikali.
Hili limefanya iwe vigumu kwa serikali nyingi kutoa amri ya kupiga
marufuku matumizi yake. Hata hivyo, ni
moja ya vitu vyenye kujenga hali ya juu sana ya mazoea au uraibu, ni sumu kwa
mazingira na mwili, na leo inabakia kuwa ni kisababishi cha magonjwa yanayoweza
kuzuilika na vifo kabla ya wakati ulimwenguni kote.
Epidemiolojia
Ripoti ya utafiti wa kiulimwengu kwa vijana wanaovuta sigara
huko Kenya 2006, ulikuwa na picha hii ya kusikitisha ya hali ya tumbaku nchini
Kenya:
· Nchini Kenya watu milioni 1.1 walio chini ya
umri wa miaka 18 walikuwa ni waraibu wa tumbaku.
· Wakenya wanavuta sigara bilioni 10 kila mwaka,
ambazo ni sawa na zaidi ya sigara 500 kwa kila mtu mzima kwa mwaka, ambayo ni
sawa na sigara 2 kwa kila mtu mzima kwa siku.
Asilimia 65.7 ya watu nchini Kenya wanavuta sigara.
· Kodi ya tumbaku inaingiza shilingi za Kenya
bilioni 5 kwa mwaka, lakini inagharimu mara tano zaidi katika gharama za
matibabu.
·
Asilimia 13-15 ya wanafunzi wa umri chini ya
miaka 15 wanavuta sigara.
·
Asilimia 44.8 ya vijana wa umri wa miaka 18-29 ni
wavutaji wa asilimia 52 ya wanavyuo na vyuo vikuu wanavuta.
·
Asilimia 30 ya watoto (milioni 1.5)
wanahatarishwa kwenye moshi wa sigara nyumbani kwao. Asilimia 80 ya wavulana na wasichana
waliohojiwa kwenye utafiti wameona matangazo yanayohamasisha uvutaji kwenye
magazeti na majarida.
·
Asilimia 50 ya wavutaji na asilimia 20 ya
wavutaji wapya walikuwa na vitu kama tisheti, kofia au kalamu zenye nembo ya
sigara.
· Asilimia 25 ya watoto walifikiria kuwa wavulana
na wasichana wanaovuta wanaonekana kuvutia zaidi. Watangazaji wanahusisha kuvuta kuvuta sigara
na kuwa mtulivu, kuchukua majukumu na kukua.
(Utafiti huu ulifanywa na Wizara ya Afya na Elimu kwa msaada wa WHO).
Sigara siyo aina pekee ya tumbaku yenye hatari. Hata tumbaku isiyo na moshi kama vile ugoro,
na zile zinazotafunwa zinazo hatari nyingi za kiafya kama sigara.
Patholojia (Kiiini,
asili, na sababu ya ugonjwa)
Tumbaku iliyokaushwa bila kuchomwa ina: Nikotini, viajenti
vinavyoweza kusababisha kansa, na sumu zingine ambazo zinaweza zikasababisha
magonjwa ya fizi na saratani ya mdomo.
Wakati inapounguzwa moshi unaotokea unakuwa na nikotini, carbon monoxide
na zaidi ya michanganyiko mingine 4000.
Moshi huo unayo zaidi ya michanganyiko 40 inayosababisha saratani. Kinachosalia baada ya nikotini na mvuke
kuondolewa kinaitwa lami. Mkupuo wa
mvuke unakuwa na Carbon monoxide, vitu vinavyowasha kwenye mfumo wa hewa, sumu
za njia za hewa na michanganyiko mingine inayoweza kufukizwa kama hewa.
Nikotini ndiyo sumu kuu na inayojenga mazoea (uraibu) katika
sigara. Ni mchanganyiko
unaosisimua. Dozi inayoweza kusababisha
kifo ni miligramu 40 au tone moja la nikotini halisi: ambalo ni sawa na kiwango
kinachopatikana katika sigara mbili. Nikotini
halisi isiyochanganywa na kitu cho chote ni sumu kali sana ambayo katika dozi
ya juu itasababisha mara moja – shinikizo juu la damu, mapigo ya moyo yasiyo ya
kawaida, kupooza kwa misuli na kushindwa kupumua, mtukutiko wa maungo au
degedege, kupoteza fahamu na kifo.
Nikotini ni moja ya vitu vyenye kujenga uraibu na kudhuru
kwa siri. Ni kwa sababu mwili hujifunza
kuchukuliana nayo kwa haraka na wengi wa watumiaji wanakuwa na uchu wa muda
mrefu wanapojaribu kuacha. Hii ndiyo inayosababisha
kujenga uraibu wa tumbaku.
Usugu wa sumu ya tumbaku na nikotini unahusika na orodha
ndefu ya magojwa:
Magonjwa yanayo
husiana na uvutaji wa sigara
1.
Mfumo wa
moyo na mishipa ya damu:
Kariia asilimia 30 ya zaidi ya vifo 500,000
vinavyotokana na maradhi ya ateri za moyo vinahusishwa na uvutaji wa
sigara. Idadi kubwa ya magonjwa ya
mishipa ya damu ya kwenye moyo, shtuko la moyo na kufa sehemu ya msuli wa moyo
husababishwa na ateriosklerosisi (ugonjwa wa mishipa ya ateri ambapo kuta zake
huwa nene, ngumu na zilizopoteza uwezo wake wa kutanuka na hivyo kipenyo chake
pia kupungua).
2.
Kiharusi:
Uvutaji sigara
takribani unaongeza maradufu hatari ya mtu kupata kiharusi. Uharibifu wa mishipa yako ya ateri inaongeza
mkusanyiko wa “plateleti” zinazohusika na kuganda kwa damu, na hivyo kuziba kwa
mishipa ya damu na hayo hupelekea kupata kiharusi.
3.
Saratani:
Uvutaji wa tumbaku unasababisha idadi kubwa
ya saratani ya mapafu. Uvutaji wa sigara
unasababisha asilimia 90 ya vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu kwa
wanaume, na asilimia 80 kwa wanawake.
Saratani zingine zinazohusiana na uvutaji wa sigara ni ile ya zoloto,
midomo, umio, kongosho, figo, na kibofu cha mkojo.
4.
Mimba:
Wanawake wanaovuta sigara wakati wa
ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata athari zifuatazo:
- Kuachia na kuvuja damu chini ya kondo la nyuma.
- Hatari ya kuharibika mimba
- Kuzaa njiti – Watoto wachanga wana uwezekano mkubwa wa kufa baada tu ya kuzaliwa kwao, ni wadogo kulinganisha na umri wa mimba, wana mwelekeo zaidi wa vifo vya haraka vya watoto wachanga na wanachelewa katika ukuaji wao.
- 5. Maradhi yanayohusiana na upumuaji:
Uvutaji tumbaku unahusiana sana na maradhi
ya upumuaji. Asilimia 90 ya maradi sugu
ya kuziba kwa njia ya hewa inasababishwa na uvutaji na pia inahusika na
asilimia 20 ya vifo vyote.
6.
Matatizo
mengine:
Uvutaji wa sigara unaathiri karibu kila kiungo
cha mwili, kwa mfano: maradhi ya macho kama mtoto wa jicho uzeeni, mabadiliko
kwenye retina. Ngozi (kuwa na kunyanzi
mapema) na tumbo (kuchelewa kupona kwa vidonda vya tumboni).
Wanaovutishwa moshi
wa sigara
Madhara ya kiafya ya wanaovutishwa moshi wa sigara karibu ni
sawa tu na yale ya wavutaji. Wale ambao
kila wakati wako karibu na moshi wa wavutaji (wanaovutishwa au wavutaji baridi)
wanakabiliwa na hatari zifuatazo kiafya:
- Maradhi ya ateri za moyo
- Saratani ya mapafu
- Maambukizi katika mfumo wa upumuaji
- Pumu
Uraibu (Mazoea sugu)
Tumbaku ni yenye kufanyiza uraibu. Inafikiriwa kuwa inabadilisha hali na
mwenendo. Tumbaku inaaminika kuwa na
nguvu ya kujenga uraibu iliyo sawa na pombe, kokeini na afyuni. Kwa tafsiri uraibu ni ugonjwa sugu.
Usimamizi
Uvutaji sigara ndiyo sababu inayoongoza ya vifo na maradhi
yanayozuilika ulimwenguni, na sababu kuu ya vifo vya mapema ulimwenguni
kote. Ziko njia mbalimbali za kuweza
kushughulika:
Kitabibu
1. Wanaweza
wakaitikia tiba mbadala ikichanganyika na nikotini kidogo.
2. Kuondoa
sumu kwa kutumia Clonidine
3. Bupropion
– inayotuliza mfadhaiko
4. Mecamylamine
– inazuia nikotini kupokewa na seli na inayofika vizuri katika mfumo wa
neva. Ina kikomo cha kufaa kwake. Kasi ya mafanikio jumla kwa kuacha kabisa kwa
mwaka mmoja ni asilimia 20.
Kuna mafanikio kidogo kwa wavutaji wenye
mfadhaiko.
Uzuiaji
Njia pekee inayofaa sana kupambana na uvutaji sigara ni
kuzuia uvutaji.
Elimu na sera za serikali za kusimamia
uzalishaji, uuzaji, matumizi na matangazo vinakwenda pamoja. Jambo bora zaidi ni kuwa kamwe usivute sigara
ya kwanza. Kutokana na ujinga na
ushamba, vijana wengi wanakuwa mateka wa mazoea ya kuvuta tumbaku. Watengenezaji wanafanya matangazo yanayovutia
na yenye kutamanisha sana yakiahidi furaha ya ajabu na maisha yenye kuridhisha,
yaliyojaa fahari. Lakini ni waangalifu
sana kiasi kwamba hawawezi kukwambia ukweli wote.
No comments:
Post a Comment