Asali ni chakula muhimu ambacho kwa muda mrefu kimekuwa
kikisaidia kuongeza ladha ya mlo. Wapo
wanaoitumia kwenye chai, maziwa au kahawa wengine wakiipaka kwenye mkate na
baadhi wakiweka kwenye uji wa mtoto au juisi ya familia.
Kwa mujibu wa tafiti za dawa lishe matumizi ya kila siku ya
asali yanapunguza kiwango cha lehemu mwilini huku ikisaidia kupambana na
magonjwa yatokanayo na uzee.
Waaustralia na Wajapan wanasema asali ina uwezo wa kumpa
nafuu mgonjwa wa saratani. Licha ya
faida hizi chache bado asali hufanya kazi nyingi mwilini ikiwamo kuimarisha
kinga za mwili.
Asali, ikipakwa sehemu husika, ina uwezo wa kulainisha jipu
na kuondoa usaha. Vilevile, hutuliza
maumivu ya tumbo na kurahisisha umeng’enyaji wa chakula huku ikisaidia kutibu
vidonda hasa vitokanavyo na majeraha ya moto.
Asali ni msaada kwa wenye matatizo ya kifua na mapafu. Asali inazuia ugumba na inaamsha hisia za
kufanya mapenzi. Wataalamu wanashauri
wapenzi kunywa walau vijiko viwili vya asali kila siku kabla ya kulala usiku
ili kuimarisha uwezo wao wa kushiriki tendo.
Asali kutibu mafua. Wataalamu
mbalimbali wa tiba mbadala wanasema kuilamba yenyewe au ikichanganywa na baadhi
ya vitu vingine huwa ni tiba tosha ya mafua.
Mchanganyiko wa kijiko kimoja cha asali, mdalasini kwenye
kikombe kimoja cha maji ya uvuguvugu unasaidia kuondoa chafya na uvimbe wa koo
pia.
Asali ni tiba kwa ngozi ya uso na huwasaidia wenye vidonda
vya tumbo. Hutibu maumivu ya jino,
maambukizi ya kibofu cha mkojo, fangasi za miguu na upungufu wa nguvu za kiume.
Hupunguza uzito pia.
Sukari ya asili iliyomo kwenye asali huondoa uchovu hasa kwa wazee.
Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha
Washington, Marekani wanaeleza sumu ya nyuki inaponya maradhi mbalimbali ikiwamo
kupunguza nguvu ya virusi vya Ukimwi bila kuharibu seli za mwili. Wanasayansi hao wanaeleza sumu hiyo iitwayo
melitin iliyomo kwenye mwiba wa nyuki ina uwezo wa kuingia ndani ya mfuko
unaozunguka kinga ya mwili wa binadamu na kufubaza virusi vya Ukimwi.
No comments:
Post a Comment