Wednesday, February 15, 2017

MADHARA YA UGONJWA WA MALARIA SUGU


Ugonjwa wa malaria sugu unaweza kusababisha kifo kwa mwanadamu ikiwa hautahangaikiwa mapema.  Lakini pia wataalam wa masuala ya afya wanaeleza kuwa yapo madhara mengine ambayo yanaweza kujitokeza haraka baada ya plasmodium kutawala mwilini.  Miongoni mwa madhara hayo ni kama ifuatavyo:

·        
Ugonjwa wa malaria sugu unaweza kusababisha matatizo kwenye afya ya akili kwa kupanda kichwani na kuleta kichaa.

·        
Uwezo wa kufanya kazi hupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na misuli kukosa nguvu ya kuwajibika.

·        
Kudhoofika mwili na kushuka kwa uzito kwa kiwango kikubwa kutokana na kujirudiarudia kwa malaria sugu kwenye mwili wa mwanadamu.

·        
Msongo wa mawazo ambao unaweza kupelekea matatizo ya moyo.

·        
Ubongo kupoteza kumbukumbu za matukio muhimu.

·        
Uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo hushuka hivyo kuathiri utendaji wa shughuli za kila siku.

·        
Wakati mwingine macho hubadilika rangi na kuwa njano pindi inapofika hatua kubwa.

Haya ni baadhi ya madhara ambayo yanaweza kumpata mgonjwa wa malaria sugu lakini bado kuna namna nyingi za kufanya baada ya kuhisi dalili kwa sababu uwezekano wa kutibika ni mkubwa tofauti na maradhi mengine sugu kama vile UKIMWI.

Mahala salama ambapo panaweza kuwa suluhisho jema ni kwenda hospitali ambako kunapatikana vipimo sahihi ambavyo vinaweza kugundua kiasi cha bacteria waliomo mwilini.

Matokeo ya vipimo vya daktari ndio njia sahihi ya kufahamu aina ya tiba kwa mgonjwa husika hivyo ni muhimu kufuata malekezo yake ili kujinusuru na madhara mengine makubwa ikiwemo kifo.

Ipo kawaida kwa baadhi ya watu kujichukulia uamuzi wa kutumia dawa za kienyeji ikiwemo muarobaini kabla ya kufanyiwa vipimo.  Wakati mwingine tiba za namna hii huleta madhara makubwa ikiwa zitafanywa bila kuzingatia miongozo ya kitaalamu.  Kumbuka kwamba matumizi ya dawa hizi kwa wingi wakati mwingine husababisha matatizo ya figo mwilini baada ya kuongezeka kwa kiwango cha sumu mwilini.

Kwa kawaida kinga ni bora kuliko tiba kutokana na gharama nyingi zinazoweza kutumika pamoja na masharti anayoweza kupewa mgonjwa ambapo wakati mwingine huwa ni magumu kuyafuata kutokana na mfumo wa maisha na desturi zilizozoeleka.
Share:

No comments:

Post a Comment