Wednesday, February 15, 2017

JINSI YA KUEPUKANA NA UGONJWA WA MALARIA SUGU

jinsi ya kuepukana na ugonjwa wa malaria sugu

Zifuatazo ni njia madhubuti ambazo zinaweza kukuepusha na kukumbwa na malaria sugu katika maisha yako.

·        
Punguza matumizi ya pombe zenye kilevi kikali kwani hupunguza uwezo wa chembe hai nyeupe kufanya kazi ya kukukinga na maradhi.

·        
Inashauriwa kutumia nyama nyeupe kama samaki na kuku

·        
Pendelea kutumia juisi ya malimao lakini usiongeze kiasi chochote cha sukari.

·        
Teketeza mazingira yote ambayo yanasababisha kuzaliana kwa mbu.

·        
Tumia chandarua kilichotiwa dawa ili kujikinga na mbu waumao nyakati za usiku.

·        
Jenga utamaduni wa kufanya mazoezi mfano; kuruka kamba, kukimbia, na kutembea ili upate nafasi ya kuimarisha afya yako.

·        
Jishughulishe na kufanya kazi za mikono kwa wingi na kutumia nguvu

·        
Kunywa maji kwa wingi ili kuimarisha uwezo wa chembe hai nyeupe kufanya kazi kikamilifu.  Jitahidi kunywa glasi zisizopungua nane kwa siku.

·        
Jiwekee utaratibu wa kula mboga za majani na matunda ili kuongeza kiasi cha vitamin “C” mwilini. 

Pamoja na uwepo wa njia mbadala za kuweza kujikinga na malaria sugu lakini pia ni vema kukumbuka masuala yafuatayo:

·        
Ugonjwa wa malaria sugu hauambukizi baina ya mtu na mtu.

·        
Ni vema kujiepusha na matumizi ya pombe baada ya kuanza dozi iwe ya kienyeji au kitaalam kwani kwa kufanya hivyo unapunguza uwezo wa dawa kufanya kazi na wakati mwingine unaweza kukumbwa na kifo au hali kuwa mbaya zaidi.

·        
Si nzuri kuchangaywa madawa ya hospitali na yale ya kienyeji kutoka mtaani kumbuka madawa yanaongeza sumu mwilini.

·        
Ni vyema kumaliza dozi uliyopewa na daktari

Unywaji wa maji mengi na mlo kamili vinaweza kuongeza uwezo wa mwili katika kusaidiana na dawa kufanya kazi kwa ufasaha.
Share:

No comments:

Post a Comment