Endapo umeanza kuhisi dalili za
kuwa na tatizo hili au umepimwa na kukutwa na tatizo hili likiwa katika hatua
za mwanzo, ni rahisi kulitibu endapo utafuata maelekezo yaliyo hapo chini.
Lakini kabla ya kuanza kufuata
maelekezo hayo, ni vyema kupata ushauri wa daktari wako kwanza juu ya uwezo wa
mwili wako kustahimili tiba za mbadala na kama utatakiwa kutumia dawa za
hospitali ni vyema kumaliza tiba za hospitali kwanza kabla ya kuanza tiba
hii. Lakini njia hizi zinafaa hata kwa
wale wanaohitaji kuzuia uwezekano wa wao kulipata tatizo hili kwa siku za usoni
hata kama hawana tatizo hilo:
1.
Fanya
mazoezi ya nguvu: Njia hii huweza
kupunguza kiwango cha mafuta kwenye moyo na mishipa ya damu hivyo huweza
kusaidia kuepukana na matatizo ya kupatwa na shinikizo kubwa la damu mwilini.
2. Epuka matumizi ya chumvi: Ni ukweli usiopingika kuwa chumvi
huongeza madini ya joto mwilini na kuleta ladha kwenye chakula lakini inapaswa
kupunguzwa kwani pia inaweza kupelekea madhara ya kupatwa na shinikizo kubwa la
damu ikiwa itazidishwa. Inashauriwa
kutotumia chumvi mbichi kwenye chakula.
3. Kunywa pombe kiasi na ikiwezekana acha
kabisa: Ulevi uliokithiri huleta
matatizo mengi kwenye afya ya mwanadamu ikiwemo mapigo ya moyo kwenda mbio na
kuchochea ugonjwa wa shinikizo kubwa la damu mwilini hivyo ni vema kuepukana na
ulevi uliokithiri.
4. Fanya kazi za nguvu: Kitendo cha kukaa kwenye ofisi kwa muda wa
masaa 41 kwa wiki bila kutoka jasho kinaweza kukuweka kwenye hatari ya kupatwa
na msukumo mkubwa wa damu hivyo ni vema wakati mwingine kufanya kazi za nguvu
ili kujiweka fiti dhidi ya maradhi kama haya.
5. Jiburudishe na muziki: Wakati mwingine msongo wa mawazo hupelekea
matatizo ya shinikizo la damu hivyo ni vema kuiburudisha akili yako na aina ya
miziki unayoipenda ili kuondoa mawazo yanayosumbua akili yako. Kwa kufanya hivi unaweza kupunguza shinikizo
kubwa la damu.
6. Jenga utaratibu wa kutembea kwa miguu: Kwa kawaida utembeaji kwa miguu husaidia
kupunguza tatizo la shinikizo kubwa la damu kwa mwanadamu. Inashauriwa walau kutembea mwendo wa nusu saa
kwa siku ili kuufanya moyo wako upate hewa ya kutosha kusukuma damu
vizuri. Jaribu kuongeza kiwango cha
kutembea kadri siku zinavyozidi kwenda.
7. Anza kutumia viazi: Matumizi ya viazi, matunda na mboga zenye
kiwango kikubwa cha potasiamu vinaweza kusaidia kupunguza tatizo la shinikizo
kubwa la damu mwilini. Tumia potasiamu
kwa kiwango cha miligramu 2,000 mpaka 4,000 kwa siku. Madini haya unaweza kuyapata kwa kula vyakula
kama viazi vitamu, nyanya, juisi ya machungwa, ndizi, maharage.
8. Tumia chocolate nyeusi: Tafiti zinaonesha kuwa matumizi ya chocolate
nyeusi husababisha mishipa ya damu kuwa minyumbufu na kusaidia kupunguza
kiwango cha msukumo mkubwa wa damu mwilini.
No comments:
Post a Comment