Friday, February 17, 2017

SHINIKIZO LA JUU LA DAMU (HIGH BLOOD PRESSURE)


shinikizo la juu la damu


Watu wengi wanafahamu madhara ya shinikizo kubwa la damu na jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo pindi linapowakumba lakini pia ni vema kufahamu kuwa shinikizo kubwa la damu lina hatari kubwa kwa maisha ya mwanadamu.
Pindi shinikizo la damu linapokuwa juu ya kiwango halisi cha 120/80 huchukuliwa kama shinikizo kubwa la damu katika mwili wa mwanadamu.
Tatizo hili hutokana na msukumo mkubwa wa damu kwenda katika moyo na ubongo.  Matokeo yake mwili hushindwa kufanya kazi kwa ufasaha na kuelemewa.
Dalili za Shinikizo Kubwa la Damu
Hakuna dalili za moja kwa moja kwa tatizo la shinikizo kubwa la damu katika mwili wa mwanadamu kwani wahanga wengi wa ugonjwa huu wamekuwa hawaoneshi ishara za wazi kama ilivyo kwa magonjwa mengine.  Lakini kitaalamu yapo mambo kadhaa ambayo yanaashiria uwezekano wa mtu kuwa na tatizo la shinikizo kubwa la damu endapo litakuwa limekomaa na kufikia hatua ya hatari kama ifuatavyo:
·         Mabadiliko kwenye mapigo ya moyo na kuwa ya juu kupita kiasi
·         Kuumwa kichwa
·         Kichefuchefu
·         Kutapika
·         Kizunguzungu
·         Kuona maruweruwe
Visababishi vya Msukumo Mkubwa wa Damu
Shinikizo la juu la damu huwa linasababishwa na vitu vingi lakini sababu zilizo kuu zinaweza kuwa mojawapo au zaidi ya hizi zilizoainishwa hapo chini:
·         Unene uliopitiliza
·         Kutokuwa na mazoezi ya kutosha
·         Msongo wa mawazo na hofu ya mfululizo
·         Matumizi ya vyakula vyenye mafuta mengi
·         Magonjwa ya figo
·         Mabadiliko ya mfumo wa homoni
·         Udhibiti mbaya wa matumizi ya sukari
·         Mshtuko wa ghafla
Madhara ya Msukumo Mkubwa wa Damu
Mara nyingi msukumo wa damu hupelekea madhara yafuatayo:
·         Shambulio la moyo (heart attack)
·         Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
·         Ini kushindwa kufanya kazi (Liver failure)
·         Kiharusi (Stroke)
·         Macho kuharibika
Mguu na mkono kuuma mfululizo
Share:

No comments:

Post a Comment