Ulaji wa yai kwa siku unaweza kuwasaidia watoto wadogo wenye
utapiamlo na kuongeza urefu hii ni kwa mujibu wa utafiti wa miezi sita huko
Ecuador.
Haijalishi yai hilo ni la kukaangwa au la kuchemshwa bali
watafiti wanasema yai ni njia isiyo ghali ya kuzuia udumavu kwa watoto.
Miaka miwili ya kwanza maishani ni ya muhimu sana kwa ukuaji
na maendeleo hivyo kudumaa kunaweza kuleta madhara makubwa kwa watoto.
Lishe duni ni sababu kubwa ya kudumaa, pamoja na maambukizi
ya utotoni na magonjwa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, watoto milioni
155 chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa.
Wengi wao wanaishi nchi zilizo na kipato cha chini na cha
kati na wataalam wa afya wamekuwa wakitafuta njia za kukabiliana na tatizo
hilo.
No comments:
Post a Comment