Hivi mtu aliyewahi kutoa mimba mara mbili na mpaka dakika
hii bado hajapata ujauzito, je hapo baadaye akipata ujauzito ataweza kuzaa
vizuri bila kupata shida yoyote? Na je atawahi au atachelewa kuzaa?
Kutoa mimba kinyume na sheria ni uondoaji wa kiumbe
kilichotungwa kabla ya muda wa kuzaliwa haujafika pasipo sababu ya kitabibu.
Ieleweke kuwa si lazima utolewaji wa mimba kuwa na
muingiliano wa uwezo wa mwanamke kupata mimba, jambo la msingi ni utoaji uwe ni
salama na usio na madhara yoyote.
Katika nchi ambazo utoaji mimba si uvunjaji wa sheria,
wanawake wengi hutolewa mimba na kuwa salama bila kujitokeza kwa madhara yoyote
baadaye huweza kupata ujauzito mwingine wakiwa tayari kufanya kwa hilo.
Endapo mwanamke aliyetoa atajamiiana bila kinga yoyote
anaweza kupata mimba nyingine ndani ya wiki mbili zitakazofuata baada ya yai
lake la uzazi kupevuka.
Mtu anaweza kutoa mimba hata mara tano na akawa na uwezo wa
kuzaa wakati wowote kama tu utoaji ulizingatia utaratibu unaotakiwa na hakuna
madhara yoyote yaliyojitokeza.
Madhara yanayoweza kujitokeza kwa kutoa mimba ni pamoja na
maambukizi ya via vya uzazi, majeraha ya mlango wa uzazi na ndani ya mfuko wa
uzazi ndiyo yanayoweza kusababisha mtu kushindwa kupata ujauzito hapo baadaye
au akipata inatoka.
Utoaji wa mimba kila mara bila ushauri wa daktari unaweza
kusababisha majeraha katika mlango wa uzazi na kuufanya kuwa dhaifu na wakati
wakubeba mimba zinaweza kutoka.
Maambukizi ya nyumba ya uzazi yanaweza yakatokea wakati au
baada ya mimba kutolewa hivyo kutokea maambukizi kwenye via vya uzazi ikiwamo
mirija kuharibika.
Kuwahi au kuchelewa kuzaa hili litategemea kama hakuna
madhara yoyote yaliyojitokeza na mizunguko ya hedhi kurudi kama kawaida.
Inashauriwa kitaalam, mwanamke aliyetoa mimba au mimba yake
kuharibika na kusafishwa apumzike kwa kipindi kati ya miezi 6 mpaka 12 au mwaka
mzima kabla ya kushika ujauzito mwingine.
Kufanya hivi ni kuupa mwili nafasi ya kujijenga upya na
homoni kurudi katika utaratibu wake wa awali.
Kumbuka, mimba inapotungwa kunatokea mabadiliko mengi mwilini ili
kuandaa mazingira ya ukuaji wa mimba iliyotungwa.
Ni muhimu kuepukana na mimba zisizotarajiwa hasa
kwa wasichana wanaosoma hii ni kutokana na changamoto zinazoweza kujitokeza
ikiwamo kuachishwa masomo au kwenda zahanati za uchochoroni kutoa mimba hiyo.
Kufanya hivi ni kuupa mwili nafasi ya kujijenga upya na homoni kurudi katika utaratibu wake wa https://photoshopcreative.co.uk/user/tuvanphathaionline kujitokeza ikiwamo kuachishwa masomo au kwenda zahanati za uchochoroni kutoa mimba hiyo
ReplyDeletekujitokeza ikiwamo kuachishwa masomo au kwenda zahanati za uchochoroni kutoa mimba hiyo https://photoshopcreative.co.uk/user/tuvanphathaionline
ReplyDelete