Tohara ni kitendo kinachokubalika kijamii, kidini na kwa
baadhi ya tamaduni.
Kwanza ni vizuri kujua tohara ni nini?
Tohara ni upasuaji wa kitabibu ambao huiondoa ngozi ya mbele
iliyochomoza kufunika kichwa cha uume.
Tohara haikuanza leo, ilianza tangu zama za kale, chanzo chake ni Imani
za kidini. Mpaka leo utaratibu huo
umekuwa ukiendelea kurithiwa wazazi ambao huwatahiri watoto wa kiume.
Tohara inaweza kufanyika kwa mtu aliyezaliwa siku ya kwanza
au ya pili. Vile vile inaweza kufanyika
nyakati za watoto wakubwa mpaka utu uzima.
Upasuaji huu huchukua dakika 10 tu kwa vijana na watoto, kwa
watu wazima huweza kuchukua dakika 30 mpaka saa moja. Jeraha huweza kupona kwa siku 5-7.
Kwa namna ilivyofunika huweza kuhifadhi unyevu nyevu na
joto, mazingira haya ni makaribisho mazuri ya vimelea kuzaliana na kuleta
madhara ya kiafya.
Mtu asiyetahiriwa, kwa ndani huzalisha vitu fulani mwilini
yenye mwonekano mweupe kama maziwa yaliyokatika, uzalishaji wa taka mwili hiyo
ambayo ni kisababishi cha saratani ya mlango wa uzazi kwa mwenza wa kike
unayeshirikiana naye tendo la ndoa bila kutumia kinga yoyote.
Vilevile, ni kisababishi cha saratani ya uume ingawa
inatokea mara chache. Hivyo
aliyetahiriwa huepushwa na mambo haya mawili.
Uwapo wa ngozi hiyo huweza kutengeneza hifadhi kwa vimelea
mbalimbali kuzaliana kirahisi ikiwamo bakteria, fangasi/yeast.
Wanaume wasiotahiriwa huweza kupata maambukizi ya VVU
kirahisi pamoja na magonjwa ya zinaa hii ni kutokana na eneo hilo kuwa na tishu
laini ambayo ni rahisi kupata michubuko.
Hupata magonjwa mbalimbali ikiwamo shambulizi la mrija wa
mkojo, uambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI), shambulizi la ngozi iliyozidi ya
uume na shambulizi la sehemu ya kichwa cha uume.
Mara kwa mara mtu ambaye hajafanyiwa tohara hupata maradhi
mbalimbali yanayochangia kupata muwasho kwenye uume, kuhisi muwasho kama moto
na kutokwa na harufu mbaya.
Tohara inakuepusha na tatizo la kushindwa kurudisha nyuma
ngozi iliyofunika uume mbele, kitabibu hujulikana kama phimosis. Faida nyingine ya
tohara ni pamoja na kuyafanya mazingira ya uume kuwa masafi hivyo pia kuongeza
mvuto na hamasa kwa mwenza wake.
Tohara inakufanya kuwa na muonekano mzuri na kukuongezea
kujiamini.
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa wanaume wasiofanya tohara
ndio wanaopata maambukizi ya VVU kirahisi, kutahiriwa kunapunguza hatari ya
kupata VVU kwa asilimia 50 – 60 kama
utajamiiana na mwanamke mwenye maambukizi.
Pia, kunapunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwamo
yale yatokanayo na virusi vya herpes na papilloma.
Madhara machache ya tohara ambayo yanaweza kujitokeza
ikiwamo maumivu, kupoteza damu, kidonda kupata maambukizi, uambukizi wa mlango
wa uume na kukereketa kwa uume.
Madhara haya machache hayashindi faida za kiafya za tohara,
ni vizuri kwa wasiotahiriwa kujitokeza ili wafanyiwe tohara.
Baadhi ya sehemu, huduma hii inatolewa bure kama
sehemu ya vita dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya VVU.
No comments:
Post a Comment