Tuesday, May 26, 2015

ULAJI WA MACHUNGWA UNAOFAA



Mbegu za machungwa hasa zile zilizochungu kama zilivyo mbegu za matunda ya epo, zina kiasi kidogo cha sumu aina ya cyanide.
Aina hii ya sumu ikiliwa kwa wingi inadhuru afya. Ndio kusema, kutafuna mbegu nyingi za machungwa ni ulaji usiofaa wa matunda hayo. Tabia hiyo inaweza kumsababishia mtu matatizo ya kiafya kwa maana mrundikano mkubwa wa sumu hiyo huathiri mwili.
Mbegu za machungwa kutokana na wingi wake wa virutubisho kama protini, vitamini, madini, mafuta na nyuzinyuzi, zinatumika katika viwanda kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwamo mafuta, dawa, chakula cha ngo’mbe na mbolea.
Katika viwanda, sumu ya cyanide huondolewa. Kila siku mwili wa mtu unatakiwa upate nyuzinyuzi vikombe vitatu, sawa na mafungu matatu ya mchicha.
Bahati mbaya watu wengi mlo wao wa asubuhi, mchana na usiku hauna vyakula vya kutosha vyenye nyuzinyuzi. Kwa hiyo, mtu akila machungwa anapaswa ale na nyama yake ya ndani. Akifanya hivyo atauwezesha mwili wake kupata kiasi fulani cha nyuzi nyuzi. Hii ni aina moja ya ulaji unaofaa wa machungwa.
Nyuzi nyuzi zina kazi nyingi tumboni ikiwemo kunyonya sumu, kupunguza mafuta aina ya lehemu, kusaidia mtu kupata choo kikubwa mara kwa mara na kuzuia kansa ya utumbo mpana.
Chembe hai zinazojenga mwili wa binadamu zinakabiliwa na hatari kubwa tatu. Kukosa chakula, kushambuliwa na vijidudu vya maradhi na kuteketezwa na kemikali za free radicals.
Free radicals ni chanzo kikubwa cha magonjwa sugu kama vile saratani na magonjwa ya moyo.
Bila ya kupenda, mwili huzalisha free radicals pale chakula kinavyotumika kuzalisha nishati, chakula kinavyo mengenywa tumboni, hewa inavyoingia mwilini na jua linavyopiga katika ngozi na macho.

Mtu anapokula mlo kamili wenye matunda na mboga za majani za kijani huupa mwili wake askari wa kupambana na free radicals, kama vile maji yanavyozima moto. Askari hao ni pamoja na vitamini C, vitamini E, beta-carotene, madini ya  selenium na manganese.
Share:

No comments:

Post a Comment