Matatizo
mengi ya kiafya hutokana na uzito uliokithiri, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa
kupata ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, na baadhi ya saratani. Lakini moja kati ya magonjwa yaliyoenea zaidi ni
kisukari ambacho tutakizingatia hapa. Zaidi
ya theruthi ya watu bilioni moja ulimwenguni wana kisukari – takribani mtu
mmoja katika kila 20 duniani! Nchi zenye
uwezekano mkubwa kabisa wa ongezeko la kisukari kufikia mwaka 2030 ni pamoja na
China, India na Marekani. Hizi zinaongoza
zingine nyingi, tajiri na maskini. Unene
uliokithikiri unaelezewa kama mtu mwenye uzito uliozidi uzito wake wa kawaida
kulingana na urefu wake kwa asilimia 20 au zaidi. Kiasi cha asilimia 20 ya watu wenye kisukari
namba 2 wana uzito uliokithiri. Maradhi haya
mawili yanahusiana kiasi kwamba wataalamu wengi wa afya huyachukulia kama
ugonjwa mmoja, ambao wanauita diabesity
(kisukari kitokanacho na unene).
Kiwango cha kisukari kimeongezeka sana kwa watu
wa kawaida katika miaka ya karibuni, kama matukio ya unene uliokithiri ambao ni
chanzo cha kwanza cha magonjwa ya kisukari yanavyoongezeka. Kila mwaka kiasi cha milioni 3.4 hufa
kutokana na matatizo yanayoletwa na kisukari.
Shirika la afya ulimwenguni linakadiria kwamba kisukari kitakuwa cha
saba katika kusababisha vifo ifikapo mwaka 2030. Kama kisukari ni adui wa kufisha kiasi hicho,
basi ni muhimu kujua namna ya kukishinda.
No comments:
Post a Comment