Ulaji saladi
ya spinachi, matunda ya apple na parachichi unaweza kumsaidia mtu kuwa na uzito
unaotakiwa kiafya.
Kabla mtu
hajaanza kula mlo wake wa asubuhi, mchana au usiku anashauriwa aanze na mboga
za majani za spinachi au aina nyingine. Ulaji
wa aina hii unamwezesha mtu kula kidogo vyakula vyenye wanga, sukari au mafuta
ambavyo vinasababisha kuongezeka uzito na unene.
Saladi ya
mboga za majani hujaza tumbo na kumfanya mtu ajihisi ameshiba na hivyo kuzuia
tabia ya kutamani kula hasa vyakula vya wanga au sukari. Mboga za majani za spinachi pia, zina
kirutubisho kinachoitwa thylakoids, ambacho kinachochea mwili kuzalisha homoni
inayopunguza hamu ya mtu kutaka kula hasa vyakula vyenye sukari.
Kuhusu matunda
ya apple, kwa siku mtu akila tunda moja ni jambo zuri. Matunda ya apple yana maji na nyuzi lishe
ambazo zinalifanya tumbo kujisikia limeshiba.
Matunda ya epo pia yana kirutubisho cha pectin, ambacho kinakifanya
chakula kilichomo tumboni kusagwa kwa muda mrefu na kumfanya mtu kujisikia
ameshiba.
Mtu akila
tunda zima la epo (siyo juisi), kabla ya mlo atajisikia hali ya kushiba na
hivyo atakula kidogo chakula cha wanga au sukari.
Kwa upande
wa matunda ya parachichi, kula nusu ya tunda hilo kwa siku kunaupa mwili mafuta
bora kiafya na nyuzi lishe ambazo zinamfanya mtu ajisikie ameshiba muda mwingi
na kutokutamani chakula mara kwa mara.
Anachopaswa kufahamu
mtu ni kwamba kula vyakula vya wanga, sukari au mafuta kwa wingi ndipo mwili
unaongezeka uzito na unene kupita kiasi.
No comments:
Post a Comment