Katika miili
yetu kuna mfumo tata wa mishipa ya damu tunayoweza kuichukulia kama mabomba
yenye ukubwa kuanzia inchi moja (sentimita 2.5) hadi madogo kabisa ya inchi
0.0002, kiasi cha kutosha cha kupitisha chembe moja tu nyeupe kwa wakati mmoja. Damu husafirisha virutubisho vyote
vinavyohitajika na kila seli katika mwili wako ili ifanye kazi sawasawa. Chanzo cha nishati kwa ajili ya seli ni
sukari sahili inayoitwa glucose. Glucose (sukari) nyingi kupita kiasi
inaweza kuziharibu seli. Kwa hiyo una
njia ya ajabu na kurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Hufanya hivyo kwa kutumia insulin, kitu kitolewacho na seli zilizo
katika kongosho.
Kisukari ni
ugonjwa sugu ambapo kiasi cha sukari kinachosafirishwa na damu hakirekebishwi
kama ipasavyo. Ama mwili hauzalishi insulin kawaida (kisukari namba 1 kinachojulikana pia kama T1DM, au
T2DM). Aina ya tatu ya kisukari inaweza
kutokea kwa wanawake wajawazito ambao waliwahi kuwa na kisukari kabla. Mara nyingi hutokea baada ya miezi mitatu ya
ujauzito. Unene uliokithiri wakati wa
mimba ni chanzo kikubwa cha unene uliokithiri kwa watoto. Pia huongeza uwezekano wa shinikizo kubwa la
damu wakati wa mimba, na matatizo mengine ya ujauzito. Watoto wanaozaliwa na akina mama wanene
kupita kiasi wana hatari zaidi ya kuwa na dosari za kuzaliwa na matatizo ya
moyo.
Kisukari wakati
wa mimba kinaweza kusababisha matatizo makubwa kwa mama na mtoto. Kiwango kikubwa cha sukari wakati wa uzazi
huathiri utendaji kazi wa seli za mtoto, jambo linalosababisha kufa kwa seli na
kuongezeka kwa kasoro kwa mtoto.
Watu wenye
kisukari mara nyingi hulalamika kuwa wanakojoa sana. Kiwango kikubwa cha sukari katika damu
huongeza mkojo. Ongezeko la upungufu wa
majimaji (na sukari) kwa njia ya mkojo huleta kiu na kuwasababisha kunywa maji
mengi kujazia. Uzito unaweza kupungua,
na uharibifu wa kudumu wa neva na mishipa ya damu unaweza kutokea. (uharibifu wa mishipa ya damu unaweza kuleta
ugonjwa wa moyo, kiharusi, na figo kushindwa kufanya kazi). Kuharibika kwa mishipa ya damu iliyoachiwa
inaweza kusababisha kukatwa kwa viungo.
No comments:
Post a Comment