Wednesday, December 30, 2015

TIKITIMAJI HUIMARISHA NGUVU ZA KIUME

Water melon juice

Wanasayansi kutoka nchini Italia wamegundua kwamba tikitimaji lina umuhimu mkubwa kwa wanaume wanaosumbuliwa na tatizo hilo, huku likiwa tiba kwa wanaume wanaohitaji kuziimarisha nguvu zao na kulinda ndoa zao.

Kwa mujibu wa gazeti la Urology lililochapishwa hivi karibuni, imeelezwa kuwa amino asidi inayopatikana katika mbegu za tikitimaji husafisha na kusafirisha damu katika mifumo ya mwili kwa haraka, usahihi na kasi kubwa hivyo kuimarisha mifumo inayosafirisha damu kwenda katika uume pasipo madhara kiafya.

Tunda hilo linaloundwa na maji kwa asilimia 92, ikiwa ni chanzo cha vitamin C na karoli 72 juisi ya tikitimaji inawafaa pia watu wanaohitaji kupunguza uzito wa miili yao na wanaotaka kutibu baadhi ya magonjwa pia.  "Ni tunda zuri kwa kuimarisha ngozi lakini si kwa ladha nzuri pekee, bali lina faida kubwa kwa mwili wa binadamu ikiwamo kuboresha nguvu za kiume," anasema Justin Lanier, wa kampuni ya Crisp County Extension WALB huko Georgia.

Timu ya watafiti kutoka chuo Kikuu cha Foggia kilichopo nchini Italia wamegundua kwamba athari zitokanazo na upungufu wa nguvu za kiume, zimekuwa ni kubwa duniani huku wanaume wengi wakikimbilia viagra ambazo pia zimekuwa zikiongeza tatizo hilo.

Uchunguzi wao walioufanya kwa wanaume 24 walio kati ya umri wa miaka 57 ambao walitumia tunda hilo kwa muda wa siku kadhaa mfululizo na kwa kadri muda ulivyokuwa ukizidi kusonga nguvu zao ziliongezeka.

"Juisi hii inatakiwa kusagwa sambamba na mbegu zake, kwani kwa kufanya hivyo kila mwanaume anapokunywa glasi moja nguvu zinaongezeka na atakapofika katika tendo huwa imara tofauti na ilivyokuwa awali," anasema Dk. Harry Bone.  Anasema kazi inayofanywa na juisi hiyo ni kusafisha njia zote za mishipa ya damu na kuiwezesha kusafiri kwa kasi kuelekea katika uume iwapo mwanaume anapata hisia.  Kazi ya namna hiyo hufanywa pia na viagra. 
Share:

No comments:

Post a Comment