Upungufu wa nguvu za kiume ni mojawapo la tatizo la kiafya linaloumiza
sana kisaikolojia wanaume wengi.
Kufahamu ukweli wa jambo hili ni moja ya nyenzo ya kuweza kukabiliana
nalo.
Ukosefu wa nguvu za kiume ni moja ya mambo ambayo yanazungumzwa
sana mitaani kila kukicha. Ni tatizo ambalo
linasababisha mifarakano katika uhusiano.
Waathirika wa tatizo hili hukumbana na kunyanyapaliwa na baadhi
ya wanajamii, ambao hudiriki hata kuwanyooshea kidole na kuwakejeli wakidhani kuwa
wamejitakia, kumbe ni tatizo la kiafya linaloweza kumpata mtu yeyote yule.
Tumewahi kusikia hata wengine wakipoteza maisha, huku chanzo
kikiwa ni kutumia dawa za kuongeza nguvu, yote ni katika harakati za kujipigania
kuepukana na tatizo hilo.
Waathirika hawa wamekuwa wakipoteza fedha nyingi na mara nyingine
hujikuta wakiingia katika matatizo makubwa ya kiuchumi, baada ya kukutana na vipeperushi
au matangazo ya dawa za kuongeza nguvu za kiume. Wengi hujikuta wakitapeliwa na waganga feki ambao
wamejaa mijini na vijijini. Katika mitaa
utaona mabango mengi ya waganga wa jadi wasio na sifa wala usajili wakijitangaza
kuwa na dawa za kuongeza nguvu za kiume.
Katika magazeti hasa yale ya udaku utakutana na matangazo madogo
yakitangaza madawa mbalimbali ya kienyeji ya kuongeza nguvu za kiume.
Baadhi ya dawa hizo haijulikani wapi yalithibitika ni salama,
na huuzwa kwa kificho na hakuna uwazi katika matibabu yao.
Lakini kukurupuka na kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume
kiholela ni hatari sana, kwani baadhi ya dawa hizo ndicho chanzo cha kuumiza mwili
na kuathiri viungo kama figo.
Tendo la kusimama linahusisha mfumo wa fahamu kama vile ubongo,
uti wa mgongo na mishipa ya fahamu, mfumo wa damu ambao ni moyo, damu na
mishipa na mfumo wa tezi zinazomwaga vichocheo kama vile homoni.
Zipo kemikali nyingi za kibaolojia za mwilini zikiwamo
protini, virutubisho na vitamin tunavyopata katika lishe, husaidia pia katika
tendo hili. Kwa kawaida sehemu za uzazi
wa kiume huwa na misuli laini kama sponji ambayo huwa na mishipa midogo mingi
ambayo imejikunja kunja kama mizizi ya mmea.
Wakati wa kusimama, damu iliyosafi humiminika kupitia
mishipa ya ateri inayotanuka kuruhusu damu ya kutosha kupita kwenda katika
misuli laini kama sponji, yenyewe huwa imetulia tuli kuruhusu damu kuingia
katika mishipa hiyo.
Wakati huohuo, ile mishipa inayotoa damu chafu kurudi
kusafishwa yaani veini, huwa zimebanwa ili damu hiyo isitoke katika misuli
laini ya uume.
Kuingia huku kwa damu na kujaa na damu ya veini kuzuiwa
kutoka, ndiko kunakofanya uume kuongeza urefu na ukubwa, yaani kuweza kusimama.
Kuna matukio ya kimwili yasiyo ya hiari yaliyomo ndani ya
mfumo wa fahamu ambayo inakinzana, mmoja hufanya kazi ya kuchochea hisia za
mwili na nyingine hutuliza hisia za mwili.
Lakini, kusimama huku hakutokei tu bali kunahitajika
kusisimuliwa vichocheo hisia ikiwamo kusikia, kuona, kuhisi harufu na utambuzi
wa hisia za tendo. Mchemko wa kupata
hisia za kujamiiana katika kituo kilichopo ndani ya uti wa mgongo, ni matokeo
ya eneo la uzazi sehemu ya kiume kusisimuliwa.
No comments:
Post a Comment