Intaneti imebadilisha namna tunavyofanya kazi,
tunavyochangamana na jamii na tunavyojielimisha. Wakati ambapo intaneti imetoa miunganiko
ambayo vinginevyo isitengenezwa kwa urahisi na watu duniani kote, vilevile
imeibua matatizo ya kisaikolojia ya kipekee kwa baadhi ya watu. Kuna swali kuhusu maana ya kisaikolojia
intaneti inayoweza kuwa nayo katika jamii yetu kwa jinsi tunavyoendelea kusonga
kutoka kwenye dunia ambayo tumekuwa tukiwajua majirani zetu na kukutana na watu
uso kwa uso kuendeleza mahusiano ya kina na watu kutoka mbali. Ndoa zimevunjika, mambo yamefanyika, na vijana
wamekuwa wakitekwa na watu waliokutana nao kwenye intaneti.
Kwa kweli, kijana mmoja alikuwa akishawishiwa
kujiovadozi na madawa na marafiki zake wa kwenye intaneti na alikufa akiwa
anawasiliana kwa njia ya intaneti kwenye hili kundi.
Kuna hisia isiyotambulika ambayo inaundwa kwa kuongea kwenye
mtandao. Unaweza kuwa kama unavyotaka
uwe, onesha kwa sana au kidogo kama unavyotaka, na usihukumiwe kwa muonekano
wako. Bila shaka, hii nayo ina maana
watu wanaweza kuwa wadanganyifu kwa wengine na kutokuwa waaminifu kuhusu wao ni
nani na nini wanataka kutoka kwako. Kwa
kuongeza, kuna mchanganyiko wa nyumbani na kazi na kuongezeka kwa tabia ya
kutojichangamana na jamii. Tafiti zinaonesha
kwamba matumizi makubwa ya intaneti yanaendana na mawasiliano kidogo kwa
wanafamilia, kupungua kwa mahusiano ya kijamii na marafiki wa eneo husika, na
kuongezeka kwa mfadhaiko na upweke.
Utafiti mmoja ulionesha kwamba kutumia intaneti zaidi ya saa tano kwa
wiki inasababisha kuwa na muda kidogo na marafiki, familia, na shughuli za
kijamii.
Kwa kweli, kuna wazo kama hilo kuhusu madhara ya kutumia
intaneti kwa muda mrefu na kuna wataalamu wa afya ya akili ambao wanapendekeza
kuongeza “matumizi ya intaneti yaliyokithiri” kama ugonjwa wa akili unaoweza
kutambulika. Je unawezaje kujua kwamba
umeathirika na matumizi ya intaneti yaliyokithiri?
Zifuatazo ni ishara za onyo:
1.
Kujishughulisha na mipango ya intaneti na kufikiria
kuhusu muda mwingine utakaoweza kuwa online.
2.
Matumizi makubwa ya intaneti kwa muda mrefu.
3.
Kushindwa kunakojirudia kujaribu kukatiza
matumizi yako ya intaneti.
4.
Kujihisi kukasirika kwa haraka, kukosa pumziko
na hali ya kununa pale unapojaribu kuacha kutumia intaneti au unapozuiwa kuwa online muda ule unaopenda.
5.
Kutokuwa na ufahamu kwamba ni muda gani unatumia
kwenye intaneti, kukaa online kuliko
ulivyokuwa umekusudia.
6.
Kuwadanganya wanafamilia na marafiki kuhusu
matumizi yako ya intaneti.
7.
Kuhatarisha ajira yako au kupoteza uhusiano kwa
sababu ya muda unaotumia kwenye mtandao.
8.
Kutumia intaneti kama njia ya kuyakimbia
matatizo yako, kukabiliana na mfadhaiko.
9.
Kukataa mialiko ya kutumia muda pamoja na
familia na marafiki kwa sababu unaona ni heri uwe online.
Bila shaka, kujibu “ndio” kwenye mojawapo ya maswali haya
haioneshi uhusiano. Hata hivyo, kama
unaweza kujibu “ndio” kwa nusu ya maswali haya, hapo unaweza kuhitaji
kuchunguza matumizi yako ya intaneti.
Hapa kuna njia unazoweza kuzitumia kuzuia matumizi ya intaneti
yaliyokithiri:
·
Amua muda kiasi gani unataka kutumia kwenye
intaneti kabla hujaanza kutumia na weka alarm kwa huo muda. Kaa kwenye huo mgao wa muda na usiseme
“dakika 5 zaidi” ambayo baadae inakuwa ni saa nzima.
·
Kuwa na mapumziko ya mara kwa mara. Tumia angalau dakika 5 ya kila saa au dakika
15 hadi 20 kwa kila saa 3 kwenye shughuli ambayo haitumii mtandao. Tembea, nyoosha mwili wako, kula kumbwe, au
sikiliza muziki.
·
Tembelea mtandao kwa kusudi na mkakati. Kujivinjari kwenye mtandao bila lengo inaweza
kupelekea kuwa online muda mrefu
zaidi kuliko ulivyotazamia.
·
Kutana na watu bila kutumia mtandao. Jiwekee ahadi kwa muingiliano wa kijamii
angalau mara moja kwa siku na mtu ambaye hayuko online.
·
Usiruhusu intaneti kuwa kituo cha uwepo wako au
ya muhimu sana, sehemu yako ya siku ya kufurahia. Jikumbushe malengo yako, vitu vya thamani, na
vitu vinavyokuvutia (interests). Njia
gani nyingine ya kutimiza malengo yako isipokuwa kupitia mtandao?
No comments:
Post a Comment