Kukoboa nafaka kama vile mahindi, ngano, mtama na uwele ni
kuondoa sehemu ya nje ya nafaka hizo.
Sehemu hiyo ni chanzo kikubwa cha nyuzi lishe, vitamin, mafuta bora
kiafya, kemikali muhimu kwa kinga ya mwanadamu zinazoitwa “antioxidants” au
“phytochemicals” na aina mbalimbali za madini zikiwamo chuma, shaba, magnesium
na zinc.
Kemikali za “antioxidants” au “phytochemicals” zinamchango
mkubwa katika ujenzi na uimarishaji wa kinga ya mwili.
Ukoboaji wa nafaka kama mahindi na ngano hupoteza kiasi cha
asilimia 50 mpaka 80 cha madini na kemikali hizo muhimu kwa kinga ya binadamu
na wanyama.
Vyakula vilivyopikwa au kutengenezwa kwa kutumia unga wa
dona au nafaka zisizokobolewa mtu akila zinapandisha kiwango cha sukari katika
damu polepole na madhara yake ni madogo.
Ndio kusema pale tumboni chakula baada ya kumeng’enywa huingizwa katika
mishipa ya damu. Kasi ya sukari kuingia
katika mishipa ya damu kutoka tumboni ni kubwa kama chanzo cha vyakula
vilivyokobolewa. Mwili wa mwanadamu
huzalisha dawa ya insulin ili isaidie kuichukua sukari iliyoongezeka katika
mishipa ya damu mara baada ya mtu kula chakula.
Hali hiyo inaweza kuathiri utendaji kazi wa kongosho na
kusababisha mwili kuwa na mfumo wa kupima insulin hivyo kusababisha hata
inapokuwa ya kutosha kwenye mfumo wa damu kazi ya kubadili sukari iliyozidi ili
ipokelewe na seli, inashindikana. Mfumo
wa damu kuwa na sukari kwa muda mrefu mara kwa mara husababisha magonjwa kama
kisukari, kuongezeka lehemu, shinikizo kubwa la damu, kupata uzito na unene
kupita kiwango, magonjwa ya moyo, kiharusi na baadhi ya saratani.
Lakini wakati wa kuandaa, mfano mahindi ya dona yaandaliwe
ili kuyafanya kuwa safi kama vile kuyapembua na kuyaosha kama kuna sulu ya
kuhifadhi iondolewe kabisa.
No comments:
Post a Comment