Tuesday, August 30, 2016

KUIFIKIA AFYA YA KISAIKOLOJIA

achieving psychological health


Hali ya “kuwa vizuri kihisia” na “afya ya kisaikolojia” vimekuwa vikitumika kwa pamoja kuelezea jinsi watu wanavyofanya kazi katika upendo na utambuzi wa ulimwengu wa maisha yao.  Afya ya kisaikolojia huhusisha jinsi watu wanavyoonesha hisia zao, kukabiliana na msongo, shida na mafanikio, na kukabiliana na mabadiliko ya kwao wenyewe na mazingira yao, pia utambuzi wa kazi – jinsi watu wanavyofikiri na kutenda kwa kuunganishwa na hisia zao.  Kuna mjadala unaohusu iwapo mawazo hushawishi hisia au hisia hutusababisha kufikiri na kutenda katika njia Fulani.  Hatahivyo, mtazamo unaokubalika Zaidi ni kwamba jinsi tunavyofikiri kunaweza kubadilisha moja kwa moja jinsi tunavyohisi kuhusu kitu Fulani kwa kubadilisha mtazamo wako kuhusu hali Fulani.  Hii ina maana ya kwa jinsi gani tunaweza kuongeza kujithamini kwetu na uwezo wa kujiamini na kuboresha kujumuika na wengine. 
Share:

No comments:

Post a Comment