Monday, November 21, 2016

ZABIBU NI KINGA YA MARADHI YA MOYO

faida za zabibu

Zabibu ni miongoni mwa matunda yenye madini lukuki ikiwamo potasiamu, kopa, Vitamini A, faiba, Vitamini B1, lakini madini mengi katika tunda hili ni Vitamini C, ipo kwa asilimia 59.

Kutokana na wingi wa madini wa Vitamini C katika tunda hilo, mlaji ana uhakika wa kujikinga na maadhi ya moyo, shinikizo la damu kiharusi na damu kuganda.

Faida kubwa ya Vitamini C mwilini ni kusaidia kupunguza matumizi ya madini ya kalisiamu, ujenzi wa mifupa na kuta za mishipa ya damu, kufyonza madini ya chuma, kuondoa chembe haribifu mwilini, kuboresha kinga ya mwili.

Tunda hilo linabaki kuwa ni miongoni mwa matunda ambayo yakitumiwa kwa kiasi kidogo kila siku yana faida nyingi ikiwamo kusaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo humkinga mlaji na ugonjwa wa kiharusi.

Huku ikitanabaishwa, faida ipatikanayo katika juisi iliyotengezwa kwa tunda hilo ni kuzuia damu kuganda hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

Utafiti uliofanywa na wataalamu wa afya wa nchini Uturuki ambako matunda hayo yanalimwa kwa wingi na kuchapishwa katika tovuti ya Medicalnewstoday kwa wagonjwa 850 wenye matatizo ya magonjwa ya moyo ulibaini kuwa, asilimia 60 ya watu hao waliepukana na kurudiwa na maradhi ya kiharusi, shinikizo la damu kutokana na kunywa glasi moja ya juisi ya matunda hayo kila siku.

Faida nyingine ya matunda hayo ni kumkinga mtumiaji na maradhi ya bawasiri, huku yakibainika kukinga maradhi ya ini kutokana na uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi, huku ikiimarisha afya ya figo na kuipa uwezo wa kuondoa sumu ndani ya damu.

Kutokana na kuwa na sukari ya asili matunda ya zabibu yanapunguza maumivu, uchovu wa mwili usio wa lazima, huku yakiwa kinga ya maradhi ya sukari aina ya pili.
Share:

No comments:

Post a Comment