Kumekuwa na utata mwingi katika kuchanganua chanzo halisi
cha ugonjwa wa saratani lakini mambo ya msingi ambayo yanaelezwa na wataalam wa
afya kuwa chanzo ni kama ifuatavyo:
· Matumizi ya tumbaku kwa wingi yanatajwa kuwa chanzo kimojawapo kinachoweza kumuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya mapafu, kichwa, tumbo n.k
· Mionzi mbalimbali pia inaweza kusababisha saratani kwa mhusika ikiwa haitadhibitiwa kwa ufasaha. Mfano saratani ya ngozi hutokana na mionzi.
· Unene uliokithiri wakati mwingine pia humuweka mhusika kwenye nafasi kubwa ya kupatwa na tatizo la ugonjwa wa saratani. Ni rahisi kwa chembe hai nyeupe za mtu mwenye uzito mkubwa kushambuliwa na saratani.
· Kutofanya mazoezi mara kwa mara
· Uchafuzi wa mazingira pia ni kisababishi cha ugonjwa wa saratani kwa mwanadamu. Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 90 ya matatizo ya saratani hutokana na sababu za kimazingira.
· Kemikali mbalimbali ambazo zinapatikana kwenye vyakula, vinywaji na vipodozi vinavyotumiwa na mwanadamu.
· Maambukizi
· Baadhi ya vichocheo vya mwili wa mwanadamu husababisha upatikanaji wa ugonjwa wa saratani mfano saratani ya mifupa, saratani ya maziwa n.k
· Matumizi ya chumvi kwa wingi huweza kusababisha saratani ya nyongo.
· Nyama nyekundu
· Majeraha ya mwili wakati mwingine husababisha saratani. Mfano kuvunjika kwa mfupa kunaweza kusababisha saratani ya mfupa husika.
Sababu hizo zilizotajwa hapo juu
zinaweza kuleta athari za moja kwa moja kwenye seli za mwili na kusababisha
ugonjwa wa saratani kwa mwanadamu.
Lakini ifahamike wazi kuwa ni asilimia tano mpaka kumi tu ya saratani
hutokana na matatizo ya kurithishana kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Ugonjwa wa saratani unaweza
kukabiliwa endapo itabainika kuwapo viashiria vyote vya tatizo hili ikiwa ni
pamoja na kuchukuliwa vipimo vya kitabibu.
Mara nyingi ugonjwa huu unatibiwa kwa teknolojia ya Chemotherapy, mionzi
na upasuaji kwenye eneo lililoathirika.
Uponyaji wa saratani hutegemea na
eneo lililoathirika na ukubwa wa tatizo husika.
Ugonjwa wa saratani huweza kumkumba mtu mwenye umri wowote lakini kuna
aina chache za saratani ambazo huwapata watoto wadogo zaidi kuliko rika
jingine.
Mwaka 2007, saratani ilisababisha asilimia 13 ya
vifo vya watu duniani kote lakini hivi sasa tatizo limeongezeka zaidi kutokana
na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya mwanadamu hususani kwenye mataifa
yanayoendelea.
Soma pia DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI
Soma pia DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI
No comments:
Post a Comment