Kumekuwa na ugumu kwa kiasi
kikubwa kwa mgonjwa wa saratani kubaini dalili zake na hii ni kutokana na
ukweli kwamba kujitokeza kwa dalili hizo hutegemea zaidi eneo
lililoathirika. Ni vigumu kugundua
dalili zake pindi ugonjwa unapokuwa kwenye hatua za awali mpaka pale tatizo
linapoanza kuwa kubwa.
Ugonjwa huu humuingia mwanadamu
taratibu na wengi wamekuwa hawafahamu viashiria vya mwanzoni kutokana na aina
yenyewe ya ugonjwa kutojulikana kwa kina na wahusika. Miongoni mwa viashiria muhimu vya ugonjwa wa
saratani pindi unapoingia kwenye mwili wa mwanadamu ni kama vifuatavyo:
Madhara madogo madogo
Kuna baadhi ya dalili ambazo
hujitokeza kwa mgonjwa wa saratani kutegemeana na ukubwa wa tatizo la
mhusika. Mfano saratani ya mapafu
huambatana na dalili za kukohoa, kifua kubana.
Mgonjwa wa saratani huanza kusikia maumivu makali pindi saratani
inapokuwa imekomaa lakini katika hatua za awali maumivu huwa hayajitokezi.
Dalili za kimfumo
Hizi ni dalili za moja kwa moja
ambazo huweza kujitokeza katika mwili wa mgonjwa husika wa saratani. Mfano uzito kupungua, homa, uchovu wa mara kwa
mara, mabadiliko ya rangi ya ngozi, kibofu kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha.
Dalili za Metastasis
Hatua hujitokeza pindi ugonjwa wa
saratani unapoanza kusambaa katika maeneo mengine ya mwili wa mhusika. Mabadiliko ambayo yanaweza kujitokeza katika
hatua hii ni pamoja na maumivu au kuvunjika kwa baadhi ya mifupa.
Kwa kiasi kikubwa ugonjwa wa
saratani unatokana na sababu za kimazingira huku asilimia 5 – 10 ikitokana na
matatizo ya vinasaba.
Ni vigumu kuthibitisha moja kwa
moja chanzo halisi cha ugonjwa wa saratani kwa mhusika kwani kuna sababu nyingi
zinazopelekea athari hizo. Kwa mfano
saratani ya mapafu inahusishwa moja kwa moja na matumizi ya tumbaku lakini bado
kuna watu wanapatwa na tatizo hili pasipo kutumia tumbaku.
Ugonjwa wa saratani umegawanyika
kutokana na athari zake kwenye seli za mwili wa mhusika kama ifuatavyo:
Carcinoma: aina hii ya
ugonjwa wa saratani huwakuta watu wenye umri mkubwa na mara nyingi athari zake
huonekana kwenye maziwa, mapafu, utumbo n.k
Saacroma: aina hii ya
ugonjwa wa saratani hujitokeza kwenye maungo ya mwili wa mwanadamu mfano katika
mifupa.
Lymphoma na leukemia: haya
ni matabaka mawili ya ugonjwa wa saratani na athari zake huonekana kwenye mfumo
wa damu na mara nyingi huwakuta watoto.
Germ cell tumor: aina hii ya
saratani huathiri moja kwa moja mfumo wa uzazi.
Blastoma: saratani hii pia
huwakumba watoto wadogo kuliko watu wazima.
Ugonjwa wa saratani kwa kiasi
kikubwa unaweza kuzuilika ikiwa visababishi vyake vitakabiliwa ipasavyo na
wanadamu. Asilimia 30 ya vifo vya
saratani ambavyo vimetokea kulikuwa na uwezekano wa kuvizuia visitokee kwa
kuzingatia masuala yafutayo:
· Kuepuka matumizi ya tumbaku, ugoro na mihadarati aina ya bangi.
· Kufanya mazoezi ili kuepuka unene uliozidi kipimo.
· Kuepuka vilevi vikali.
· Kuweka mazingira safi na salama kwa mwanadamu kuweza kuishi.
· Kuepuka matumizi ya vyakula vyenye kemikali zenye sumu mfano; nyama nyekundu zilizosindikwa viwandani.
· Kuepuka matumizi ya vipodozi vikali ili kujilinda dhidi ya saratani ya ngozi.
· Kula vyakula vya asili ambavyo havitokani na mbolea za viwandani.
Zingatia
Si kila saratani inaweza kuzuilika kwa jitihada
za binadamu bali ni baadhi tu kwani vyanzo vya ugonjwa huu ni vingi. Mfano mzuri ni saratani ya kurithi ambazo ni
vigumu kukwepeka kutokana na kurithiwa na wazazi. Hata hivyo aina ya maisha anayoishi mtu na
mazingira anayoishi huweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuepukana na tatizo hili
ingawa si kwa asilimia mia moja. Mambo
kama uchaguzi wa vyakula, vinywaji, kuepukana na matumizi ya sigara, ugoro na
chumvi kwa wingi ni kati ya mambo yanayoweza kumsaidia mtu kuepukana na kansa
za aina nyingi.
Soma pia TIBA ZA ASILI ZA UGONJWA WA SARATANI
Soma pia TIBA ZA ASILI ZA UGONJWA WA SARATANI
No comments:
Post a Comment