Monday, February 13, 2017

DALILI ZA UGONJWA WA PUMU

dalili za ugonjwa wa pumu

Dalili za magonjwa ya pumu hazitofautiani kutokana na vyanzo vyake bali zote hufanana na kujitokeza sawa katika mwili wa mwanadamu pindi tatizo linapoibuka kwenye afya ya mhusika.  Fuatilia dalili zifiatazo kabla ya kuchukua uamuzi wa kufika kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi wa kina:

·        
Kifua kubana

·        
Kikohozi kikavu

·        
Mapigo ya moyo kwenda mbio

·        
Kukosa hewa ya kutosha kwenye mrija

·        
Kuhisi baridi

Zingatia

Mpaka hivi sasa hakuna dawa ya moja kwa moja ambayo imegundulika ili kuweza kutibu aina yoyote ya tatizo la pumu, ingawa kuna spray na sindano za kutuliza shambulio la pumu, lakini taarifa nzuri iliyopo ni kwamba hali zote za ugonjwa huu hata kama ipo juu au chini, inayosababishwa na mzio aua hata ile isiyosababishwa na mzio zote zinakabilika ikiwa masharti yatazingatiwa na muathirika.

Madaktari waliobobea katika kutibu ugonjwa wa pumu wanaweza kuwa na msaada mkubwa kwa mhusika wa tatizo.  Kila mgonjwa anapaswa kumuona daktari ili kufahamu mzizi wa tatizo lake na ukubwa wake kabla ya kujichukulia maamuzi ya kutumia dawa pasipo maelekezo.

Baada ya ugonjwa kugundulika, ni rahisi kwa mgonjwa kuanza tiba mbadala ili kukabiliana na tatizo kutokana na ushauri wa kitalam aliopewa.

Mgonjwa wa pumu pia anapaswa kuelewa kwamba dawa zote zilizopo duniani haziwezi kumsaidia kukabiliana na taizo lake ikiwa anavuta sigara, bangi au kutumia tumbaku.

Njia kuu ya kufanya ni kuepuka visababishi vyote ambavyo vinaweza kuchochea hali kuwa mbaya zaidi.
Share:

No comments:

Post a Comment