Jopo la wataalam wa masuala ya afya nchini Marekani kipindi
lilitoa takwimu kuhusiana na tatizo la ugonjwa wa pumu katika taifa hilo na
duniani kwa ujumla.
Tafiti zinaonesha kuwa, Marekani ilikuwa na wagonjwa milioni
17 wa pumu tofauti na miaka mitano kabla kwani waathirika walikuwa milioni
14.5.
Pumu ni miongoni mwa magonjwa sugu ya hewa yanayosumbua
idadi kubwa ya watu duniani na hasa watoto ambao wanakadiriwa kufikia zaidi
milioni 5.5 huku idadi hiyo ikiongezeka siku hadi siku.
Lakini, pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, bado kuna tumaini
juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huo kutokana na tafiti mbalimbali ambazo
zinaendelea kufanywa na wataalamu wa masuala ya afya huku wakitoa suluhisho la
kupunguza kikwazo hicho.
Uelewa wa Pumu
Pindi unapovuta pumzi, hewa huenda kwenye mdomo au pua
kupitia katika mirija ya hewa na kusafiri hadi kwenye mapafu. Katika mlolongo huu wa usafirishaji hewa
kupitia mirija yake, tatizo la pumu huibuka pindi njia hizo zinapoingiliwa na
kitu kutoka nje na kusababisha ugumu katika upumuaji.
Hali hii ya ugumu katika kupumua hujitokeza kutokana na
kubana kwa mirija ya hewa kunakotokana na kubadilika kwa utendaji kazi wa
viungo hivyo kunakotokana na kuchochewa na kitu kilichoingia kutokea nje iwe
hewa chafu, vumbi au chavua ambacho huchochea kuundwa kwa sumu katika mwili wa
mhusika huyo tu hata kama kitu hicho hakitakuwa na madhara kama hayo kwa mtu
mwingine endapo kitaingia kwa njia ya hewa katika mirija yake ya hewa
anapopumua. Kitu hiki ndicho
kijulikanacho kama Mzio au Aleji.
Kwa kiasi kikubwa tatizo la pumu hupatikana kwa njia ya
kurithi na hasa kwa wale wenye matatizo ya mzio(aleji).
Aina za Pumu
Ugonjwa wa pumu umegawanyika katika makundi mawili huku kila
moja likiwa na chanzo tofauti na lingine.
Aina ya kwanza ya ugonjwa huu hutokana na matatizo ya
kurithi na hasa kwa wale watu wenye matatizo ya mzio (aleji), hivyo hufahamika
kwa jina la allergic asthma ambavyo
imesambaa sana kwenye nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania.
Aina hii ya pumu kwa kiasi kikubwa husababishwa na
chavua(pollen), ukungu(Fog), wanyama, chembechembe za vumbi n.k. Hata hivyo mizio mara nyingi hupatikana
karibu kila sehemu. Wakati chembechembe
za vumbi na ukungu huingia kwa mwanadamu kupitia njia ya hewa, bado pumu ya
mzio inaweza kuingia mwilini kupitia kitu chochote kilicholiwa mfano matunda
aina ya strawberries.
Ukungu na vumbi lililo katika midoli pamoja na manyoya ya wanyama wa kufugwa wenye kupendeza ni hatari kwa
mtu mwenye pumu kwani huchochea shambulizi la pumu ya mzio au Allergic asthma.
Aina ya pili ya ugonjwa wa pumu hufahamika kwa jina la
(nonallrgic asthma), ambayo haitokani na matatizo ya mizio au kurithi kutoka
kizazi kilichopita hivyo huweza kumkumba mtu yoyote kutokana na vyanzo
vyake. Ugonjwa huu husababishwa na hewa
kavu, baridi kali, mazoezi, moshi, manukato yenye harufu kali, msongo wa mawazo
na kadharika.
Uchafuzi wa mazingira na moshi utokanao na uvutaji wa sigara
pia huchochea shambulizi la pumu.
Soma pia DALILI ZA UGONJWA WA PUMU
Soma pia DALILI ZA UGONJWA WA PUMU
No comments:
Post a Comment