Monday, February 13, 2017

NJIA ZA KUFANYA BAADA YA KUGUNDULIKA UNA PUMU


Mgonjwa anapaswa kumuona daktari ili kufanyiwa vipimo vya kina na kugundua chanzo cha tatizo lake na jinsi ya kukabiliana nalo.  Ushauri wa daktari utatokana na matokeo ya kipimo cha “cytotoxicity” ambacho kitamsaidia kujua aina ya mzio uliopo mwilini na kusababisha tatizo la pumu kwa mgonjwa.

Matokeo ya vipimo vyake yatasaidia kujua aina ya vyakula anavyopasa kula, dawa na maeneo hatarishi unayopaswa kuyaepuka ili kukabiliana na pumu.

Ni vema kuepuka matumizi ya dawa za kienyeji ambazo hazijathibitishwa na kitengo cha tiba za asili Muhimbili lakini pia inapaswa kuzingatia vipimo kabla ya kufanya maamuzi ya kuanza kutumia dawa.

Soma pia JINSI YA KUTIBU MATATIZO YA PUMU
Share:

No comments:

Post a Comment