Thursday, February 16, 2017

TIBA ZA ASILI ZA UGONJWA WA SARATANI


tiba za asili za ugonjwa wa saratani


Kuna vyakula na matunda yenye uwezo wa kupambana au kuzuia ugonjwa wa saratani, lakini ufanisi wake hutegemea ukubwa wa tatizo hivyo mgonjwa anapaswa kupitia hospitali ili kupata ushauri na vipimo vinavyostahili kabla ya kuamua kutumia tiba hii.  Pia ieleweke kuwa tiba zilizoainishwa hapa hazipaswi kusimama kama mbadala wa tiba za hospitalini au ushauri wa daktari ingawa utafiti unaonesha kuwa zinasaidia katika kupambana na tatizo hili kwa asilimia kubwa.
Yafuatayo ni matunda na vyakula vilivyo na uwezo wa kuzuia au kutibu saratani:
Tunda la Stafeli na Mtopetope
Matumizi ya tunda la stafeli na mtopetope mara kwa mara huweza kutibu na kuzuia saratani kwa kiasi cha mara 1000 zaidi ya tiba fulani fulani za hospitalini, hivyo tunda hili linapaswa litumike kila siku angalau mara 2 kwa kutwa.
Kabeji
Andaa juisi ya kabeji kwa kuisaga kwenye mashine ya kutengezea juisi kisha uinywe bila kuichuja kwa kipimo cha vikombe 3 mpaka 4 kwa siku.  Juisi hii huweza kuuzuia mwili usipate saratani za aina mbalimbali na pia inafaa kwa wagonjwa wa saratani walioanza matibabu.
Tunda la Parachichi
Tunda la parachichi litumike kwa wingi kutokana na uwezo wa kuzuia kufyonzwa kwa mafuta yanayoweza kusababisha saratani katika mwili.  Pia matunda haya yana kiasi kikubwa cha potasiam ambayo ni nyingi kuliko ya kwenye ndizi na pia ni chanzo kikubwa cha beta-carotene.  Wanasayansi wana amini kuwa tunda hili linatibu hepatitis ugonjwa ambao unaweza kusababisha saratani ya ini pamoja na vyanzo vingine vinavopelekea kuharibika kwa ini.
Mboga za Brocoli na Cauliflower
Cauliflower
Brocoli
Broccoli na koliflawa.  Mboga hizi zina kemikali inayoitwa “endore -3-carbinol” ambayo inazuia saratani ya matiti kwa wanawake kwa kubadilisha estrogeni yenye kusababisha saratani kuwa yenye kufaa katika mwili. Broccoli hasa machipukizi yake machanga ina kemikali inayoitwa sulforaphane ambayo husaidia kuzuia saratani za aina fulani kama vile ya tumbo na makadi (Rectum).  Hivi vyote vinapaswa kuliwa vikiwa vibichi mara kwa mara na kwa kiasi kikubwa ili kupata matokeo bora.
Karoti
Mmea wa karoti una kiasi kikubwa cha beta-carotene ambayo inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata aina nyingi za saratani zikiwemo saratani ya mapafu, saratani ya mdomo, koo, tumbo, utumbo, kibofu, tezi na matiti.  Chembechembe ya falcarinol ambayo inapatikana katika karoti hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huo.  Mboga hizi zinapatikana katika masoko yote.
Pilipili
Kiungo hiki kina kemikali inayoitwa capsaicin ambayo ina uwezo wa kudhoofisha vimelea vinavyosababisha saratani na pia ina uwezo wa kuzuia saratani ya tumbo.
Vitunguu Swaumu
Vitunguu swaumu vina kemikali inayoitwa allium ambayo huboresha mfumo wa kinga mwilini na kuzidisha utendaji wa wa seli zenye kuukinga mwili na kupambana na saratani na pia huvunjavunja chembechembe zenye kusababisha saratani.  Kiungo hiki pia huwezesha kupunguza kasi ya ukuaji wa uvimbe unaosababishwa na saratani.
Tafiti zinaonesha kuwa vitunguu swaumu, vitunguu vya kawaida ama vitunguu maji na vitunguu mboga vile vyenye kuonekana kuwa na majani ya kijani huku sehemu ya chini inayokuwa ardhini ikiwa sio kubwa huwa vinapunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo na utumbo mkubwa.  Ulaji wa mara kwa mara wa vitunguu swaumu vikiwa vibichi au kwa kuvipika kiasi hupunguza uwezo wa kupata saratani ya tumbo kwa hiyo vinapaswa kuliwa mara kwa mara vikiwa peke yake au vikiwa vimechanganywa na vyakula vingine.
Madalanzi
Madalanzi, kama yalivyo machungwa na matunda jamii ya machungwa huwa yana kemikali inayoitwa monoterpenes yenye uwezo wa kuzuia saratani.  Matumizi ya tunda la dalanzi mara kwa mara huweza kuzuia kukua au kusambaa kwa saratani ya matiti.
Zabibu Nyekundu
Zabibu nyekundu huwa zina kemikali inayoitwa bioflavonoids ambazo zina uwezo wa kuzuia vimeng’enyo ambavyo vinaweza kuchochea ukuaji wa seli za saratani na kuzuia mutikio wa kinga ya mwili.
Tunda hili pia lina kemikali inayoitwa ellagic acid ambayo ina uwezo wa kuzuia vimeng’enyo vinavyotegemewa na seli zenye saratani zinazokua na hivyo kupunguza kasi ya uvimbe wa saratani.
Mboga za Majani
Matumizi makubwa ya mboga za majani zenye rangi ya kijani kilichoiva zilizoandaliwa kwa kupikwa kwa muda mfupi husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo.
Uyoga

Kuna aina fulani ya uyoga ambazo zina uwezo wa kusaidia mwili kupambana na saratani na kujenga mfumo wake wa kinga inayozuia kuundwa kwa kansa mwilini.
Kokwa (Karaga, macadamia, karanga, miti, korosho)
Matumizi ya aina zote za kokwa hupunguza ukuaji wa saratani.  Kokwa aina ya brazilnuts zina uwezo wa kuondoa saratani ya kibofu hata hivyo watu wengi wana tatizo la mzio unaotokana na kokwa hivyo unapaswa kutafiti kujua kama una tatizo hilo kabla ya kuanza kutumia tiba hii.
Machungwa na Malimao
Haya yana kemikali inayoitwa limonene ambayo huchochea kinga ya mwili yenye uwezo wa kuua saratani.
Mvinyo Mwekundu
Mvinyo mwekundu wenye kutokana na dhabibu nyekundu hata usipokuwa na kilevi huwa una uwezo wa kuzuia mwili dhidi ya saratani mbalimbali.  Kemikali ya polyphenois huweza kuboresha mwili kwa kuondoa vimelea vya sumu vyenye kusababisha saratani na pia hudhoofisha chembechembe zenye kusababisha saratani.
Magugu aina ya Kombu
Magugu haya ni aina nyingine za mbogamboga ambazo ni chakula chenye uwezo wa kutibu uvimbe wa saratani aina ya Lymphoma, saratani ya utumbo, seli za saratani ya damu na kuzuia saratani ya matiti.  Chakula hiki kinapaswa kuliwa kila siku kwa kiasi cha nusu kilo kwa muda wa miezi mitatu mpaka sita na mgonjwa au hadi pale mabadiliko yatakapoonekana katika hali ya mgonjwa.
Faida nyingine ya mmea huwa ni kuwa unatibu maradhi mengine mengi yanayoushambulia mwili, kuondoa chembe za sumu mwilini, kukuza kinga na uwezo wa mwili kupambana na magonjwa, kuboresha ngozi ya mwili na kuleta urembo asilia, kuboresha mzunguko wa damu, kuchochea uzazi, kudhibiti kiwango cha mafuta mabaya mwilini (Bad Cholestrol), kuongeza lishe mwilini na pia husafisha damu.
Soya
Chakula hiki hakipaswi kufananishwa na magarage yenye kutumia jina hilo pia, bali hiki ni chakula kinachotokana na mmea wa aina ya mkundekunde chenye rangi nyeupe au kahawia iliyopauka kilicho na uwezo wa kuzuia saratani ya matiti na kibofu kwa kuzuia ukuaji wa vimelea vya saratani.  Soya hupatikana kwenye maduka mengi.  Chakula hiki kiliwe mara kwa mara na kwa kiasi kikubwa kwani hutibu magonjwa mengi na huongeza lishe mwilini na kuimarisha kinga ya mwili.
Share:

No comments:

Post a Comment