Tuesday, February 21, 2017

FANYA VIPIMO HIVI KABLA MWAKA HAUJAISHA




Vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza vimekuwa vikiongezeka.  Ulemavu unaosababishwa kutokana na kuchelewa kutibiwa nao ni janga la jamii.
Mfumo wa maisha na kuchelewa au kutofanya vipimo mapema au kwa wakati ni miongoni mwa sababu ya kutokea kwa yote mawili.  Hujachelewa kuanza kufanya vipimo kwa ajili ya afya hata kama huna dalili za ugonjwa wowote.
Vifuatavyo ni baadhi ya vipimo ambavyo unaweza ukavifanya kabla mwaka 2017 haujamalizika ili kujua mwenendo wa afya yako.
Uzito
Uzito uliopitiliza ni hatari kwa afya yako kwani unaongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.  Unashauriwa kufahamu Body Mass Index (BMI) yako ambayo huwianisha uzito na kimo kujua kama vinaendana na haupo kwenye hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa mujibu wa kituo cha Udhibiti wa Magonjwa nchini Marekani (CDC), mtu mzima mwenye afya njema anatakiwa kuwa na BMI kati ya 18.5 na 25.
Lehemu
Wataalamu wa afya wanapendekeza, kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 35 kupima kiwango cha lehemu au cholesterol mwilini kila baada ya miaka mitano ilikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchukua hatua na kupunguza madhara yanayoweza kuepukika.
Kwa watu wenye maradhi ya moyo, wavutaji wa sigara, wenye BMI zaidi ya 30 na wenye historia ya kupata kiharusi kwenye familia wanatakiwa kufanya kipimo hiki kuanzia wakiwa na miaka 20.
Kufanikisha kipimo hiki, sampuli ya damu kutoka kwenye mshipa wa mkono inahitajika.  Kwa viwango salama vinavyopendekezwa, lehemu inatakiwa kuwa chini ya 200 mg/dl.
Mafuta au triglycerides
Mafuta au triglycerides yanahusishwa na utendaji wa kimetaboliki mwilini na wingi wake huchangia uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya moyo, kisukari na kiharusi.
Sampuli ya damu iliyotolewa kwa ajili ya kupima lehemu inaweza kutumika kwa kipimo cha mafuta mwilini.  Inashauriwa, wingi wa mafuta usizidi 100 mg/dl ingawa kiwango chochote chini ya 150 mg/dl kinaelezwa kuwa ni salama.
Shinikizo la damu
Endapo shinikizo lako la damu lipo juu unahitaji matibabu ili kukuepusha na magonjwa ya moyo, maambukizi ya kibofu na kiharusi.  Kama shinikizo ni la kawaida, unahitaji kufanya vipimo kila baada ya miaka miwili ili kujua maendeleo yako, wataalamu wanashauri.
Kwa viwango vya kitabibu, shinikizo la kawaida huwa chini ya 120/80 mm Hg. Kama shinikizo lako lipo juu, utahitaji vipimo mara kwa mara ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
Vipimo vya shinikizo la juu huchukuliwa mara mbili kwa tofauti ya saa nne.  Hii ni kwa sababu shinikizo lililo juu ya 120/80 mm Hg huhitaji kuthibitishwa na kipimo kingine baada ya kile cha awali kilichoonesha hiyo.
Kisukari
Shinikizo la damu zaidi ya 135/80 mm Hg huwa ni dalili ya kisukari ambacho hupimwa kwa kuchukua sampuli ya damu pia.  Vipimo kadhaa vinaweza vikafanywa kubaini ugonjwa wa kisukari.
Kama ilivyo kwa shinikizo kubwa la damu, kipimo kimoja cha kisukari hakikidhi kuthibitisha ugonjwa huu.  Awamu ya pili ya kipimo cha kisukari huthibitisha kama kweli sukari yako imezidi viwango vinavyoshauriwa.
Saratani ya utumbo
Kwa mujibu wa takwimu za dunia, saratani ni ugonjwa unaoongoza kwa kusababisha vifo miongoni mwa yasiyoambukiza.  Ni wa pili kwa kufanya hivyo pia kati ya yote.
Kwa watu wenye zaidi ya miaka 50 wanashauriwa kufanya kipimo hiki haraka ili kuchukua hatua stahiki mapema kabla madhara yake hayajawa makubwa.
Kipimo chake kiitwacho colonoscopy hakina maumivu na huchukua kati ya dakika 15 na 20 kutoa majibu yanayotakiwa.  Habari njema ni kwamba, kipimo hiki kinaweza kugundua saratani hata ikiwa katika hatua zake za awali kabisa na matibabu yakafanyika.
Saratani ikigundulika mapema, madaktari wanaweza kudhibiti kusambaa kwake hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuchukua hatua.
Msongo wa Mawazo
Maambukizi ya saratani ya ngozi au melanoma yameongezeka kwa kasi ndani ya miongo minne iliyopita.  Ni miongoni mwa saratani zinazowashambulia zaidi wanaume.  Kabla ya miaka 50, wanawake wengi hupata maambukizi ya saratani hii lakini baada ya miaka 65 hali huwa kinyume chake, wanaume hupata maambukizi haya zaidi kuliko wanawake.  Baada ya miaka 80, wanaume hupata maambukizi mara tatu kuliko wanawake.
Inashauriwa kuchunguza ngozi kila mwezi ili kubaini dalili zisizo za kawaida.  Aina fulani ya vipele au vinundu viitwavyo moles hujitokeza ambavyo husababisha rangi ya ngozi kubadilika, huwa na kipenyo cha zaidi ya milimita tano.
Moles pia huweza kuwa na maumivu, kutoa damu au kubadilika kwa namna yoyote.
Kama unapata vidonda visivyopona au vinavyochelewa kupona kwa muda mrefu unahitaji uchunguzi wa daktari kuona kama ni saratani ya ngozi ambayo hutibika ikigundulika mapema.
Share:

No comments:

Post a Comment