Nanasi ni tunda linalopatikana kwa wingi nchini ingawa wengi
hawafahamu umuhimu wake katika kuimarisha kinga za mwili, ili kujiweka mbali na
maambukizi ya magonjwa kutokana na kupungua kwa kinga za mwili unashauriwa kula
tunda hili kukabiliana na tatizo hilo.
Nanasi ni moja kati ya tunda lenye ladha nzuri mdomoni
lakini lina vitamin nyingi na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuupa mwili
nguvu na kuepuka kushambuliwa na maradhi.
Kwenye tunda hili kuna kirutubisho aina ya bromelain ambacho
hulifanya nanasi kuwa muhimu katika kujenga na kuimarisha kinga ya mwili.
Ulaji wa mara kwa mara wa tunda hili husaidia kuimarisha
kinga za mwili ambazo hukabiliana na kuvimba koo, ugonjwa wa baridi yabisi,
ugonjwa wa gauti na hutibu matatizo ya tumbo ikiwapo bandama.
Wataalamu wa afya wanashauri ulaji wa tunda hilo kabla au
baada ya kula mlo ili kuimarisha kinga za mwili dhidi ya maradhi
mbalimbali. Haishauriwi kula nanasi
pamoja na chakula kingine kwa wakati mmoja.
Endapo hilo litafanywa, virutubisho vilivyopo katika nanasi
vitafanya kazi nyingine tofauti na ile iliyokusudiwa. Nanasi lina virutubisho vingi ikiwamo vitamin
A, B na C na ina madini ya chuma, shaba na phosphorous ambayo ni muhimu katika
afya ya binadamu.
Vilevile, tunda hili hutibu matatizo ya ini, homa, vidonda
vya mdomoni, magonjwa ya koo na husaidia kusafisha utumbo mwembamba.
Kwa wale wanaopoteza kumbukumbu, nanasi lina uwezo wa kutibu
tatizo hilo kwa watu wazima na vijana pia.
Mbali na faida hizo, nanasi lina uwezo wa kutibu kikohozi,
kuondoa woga, kutetemeka na baridi yabisi.
Ulaji wa nanasi mara kwa mara husaidia kutibu maradhi ya
akili, kukosa mori, kutibu matatizo ya wanawake hasa upungufu wa homoni na
matatizo mengine ya sehemu za siri za mwanamke na husaidia kupata choo laini
kwa wakati.
Tunda hilo husaidia kutibu upungufu wa damu na kuongeza
maziwa kwa wanawake wanaonyonyesha.
Nanasi pia linajulikana kwa uwezo wa kuimarisha nuru ya
macho. Utafiti unaonesha ulaji wa tunda
hili na mengine kwa kila mlo kwa siku kunaondoa hatari ya kupungua kwa nuru ya
macho kwa asilimia 36 kwa watu wazima.
No comments:
Post a Comment