Monday, February 13, 2017

JINSI YA KUBAINI VIDONDA VYA TUMBO

jinsi ya kubaini vidonda vya tumbo

Wataalamu waliobobea wanaweza kuwa na suluhisho jema katika kubaini tatizo hili kupitia namna nyingi, mfano vipimo vya X-Ray vinaonesha moja kwa moja maeneo yaliyoathirika hivyo kurahisisha upatikanaji wa dawa.

Daktari pia anaweza kupima kiasi cha bacteria ‘H. pylori’ kwa kutumia kifaa kinachoitwa fiber-optic endoscope, ambacho kitamsaidia kubaini tatizo kabla ya kutoa ushauri wa kitabibu.  Kipimo hiki hufanywa kwa kuingizwa tumboni kifaa cha kamera chenye umbo mfano wa bomba jembamba ambacho humwezesha daktari kuona vidonda vilivyo tumboni kama inavyoonyeshwa hapo chini.

Ni vyema kufanyiwa vipimo kabla ya kuchukua uamuzi wa kutumia madawa baada ya kuhisi dalili.

Mambo ya kuzingatia ili kuepukana na tatizo la vidonda vya tumbo
         i.            Epuka matumizi ya sigara au tumbaku ili kujikinga na athari za kupata vidonda vya tumbo.  Sigara na tumbaku zina kemikali inayoitwa Nicotine ambayo inaweza kukusababishia vidonda vya tumbo.  Tafiti zinaonesha kuwa watumiaji wa sigara na tumbaku wana uwezekano mkubwa wa kupatwa na ugonjwa huu.
       ii.            Kula mlo kamili kwa wakati muafaka na epuka viporo.
      iii.            Punguza matumizi ya vyakula vyenye asili ya gesi kama maharagwe, njegere n.k
     iv.            Matunda yenye tindikali nyingi sio mazuri hususani kwa mgonjwa aliyeanza dozi ya vidonda vya tumbo.  Mfano wa matunda hayo ni; machungwa, ndimu, Limao n.k
       v.            Epuka kuwa na msongo wa mawazo kwani wakati mwingine hupunguza uwezo wa mwili kuzuia kiwango cha tindikali mwilini.

Tahadhali

·         matumizi ya dawa za kienyeji ambazo hazifanyiwa utafiti wa kina yanaweza kuwa na madhara makubwa zaidi kwa mgonjwa mwenye tatizo hili.

·         Ugonjwa huu hautokani na dhana ya kurogwa.

·         Ni vema kupunguza unywaji wa pombe uliokithiri.

Badili mwenendo wa maisha kwa kuanzia katika matumizi ya vyakula mpaka vinywaji.

Soma pia TIBA ZA ASILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Share:

No comments:

Post a Comment