TIBA YA MAJI
Tiba hii inafaa kwa kutibu vidonda vya tumbo vilivyo katika
hatua za awali.
Mgonjwa anapaswa kunywa lita moja ya maji masafi na salama
alfajiri kabla ya jua kuchomoza na kabla hajakisafisha kinywa chake wala kunawa
uso au kupata kifungua kinywa. Kisha
mgonjwa anapaswa kusubiri kwa dakika 45 kabla ya kupata chakula cha mchana na
asinywe maji yoyote baada ya kula chakula hicho cha mchana kwa dakika 45.
Wakati wa usiku mgonjwa anapaswa kunywa maji lita dakika 45
kabla ya kula chakula cha usiku na akae dakika 45 kabla ya kwenda kulala.
Tiba hii huchukua muda wa siku kumi mpaka mwezi mmoja kabla
ya kupata nafuu. Katika kipindi hiki
chote mgonjwa anapaswa kuzingatia masharti juu ya ulaji na vitu vya kuepukwa.
Kabeji
Kunywa juisi ya kabeji mbichi baada ya kuikatakata vipande kisha isage kwenye mashine ya
kutengenezea juisi (Blender). Baada ya
hapo pima kwenye kikombe kimoja cha chai na unywe mara nne kwa siku. Tiba hii inaweza kutibu tatizo la vidonda vya
tumbo kwa muda wa siku kumi. Kumbuka
kuzingatia masharti ya msingi yaliyoainishwa hapo juu.
Asali
Asali ina chembechembe za asili zenye kuua bacteria na
virusi ambazo vina uwezo wa kuua helicobacter Pylory ambao ni wadudu
wanaosabisha ugonjwa huu kitu kinachomaanisha kuwa ina uwezo wa kutibu vidonda
vya tumbo. Kingine ni kwamba asali
huweza kulainisha umio, mfuko wa chakula na utumbo hivyo huweza kufunika
vidonda vilivyopo tumboni. Kutokana na
kufunika vidonda maumivu ya kuchoma pamoja na dalili nyingine za vidonda vya
tumbo hupungua.
Asali pia huweza kusafisha uvimbe na kusafisha vidonda
ambavyo hujitokeza kwenye njia ya chakula.
Asali inayopaswa kutumika kwa kusudio hili inapaswa iwe mbichi na isiwe
imeongezewa vitu vingine na dozi yake ni vijiko vya chakula viwili mpaka vitatu
kwa siku.
Vitunguu Swaumu
Viungo hivi ni tiba nyingine inayofaa sana katika kutibu
vidonda vya tumbo kutokana
na kemikali zinazoua wadudu pamoja na virusi zilizomo ndani yake na hivyo
huweza kupambana na kuua bacteria wanaosababisha vidonda vya tumbo.
Viungo hivi hufahamika kwa kusaidia katika kutibu vidonda
vya tumbo hata pale vinapotumika vikiwa vimechanganywa na vyakula vingine
kutokana na nguvu nyingi iliyomo ndani yake pamoja na chembechembe zenye
kuamsha na kuboresha mwili zilizomo ndani yake ambazo huwezesha kuukinga mwili dhidi
ya maambukizi kama vile vidonda vya tumbo.
Hivi ndivyo unavyopaswa kutumia vitunguu swaumu kwa ajili ya
kutibu tatizo hili:
Kula punje tatu mpaka nne za kiungo hicho kwa siku zikiwa
zimechanganywa na kijiko kimoja au viwili vya asali kwa siku.
Jibini Ngumu Iliyosagwa (Grated Cheese)
Kula jibini ngumu husaidia kufunika vidonda vya tumbo hivyo
hupunguza maumivu makali ya vidonda kwa hiyo iliwe kwa wingi na mtu mwenye
tatizo hili na kwa wale ambao vidonda vyao vina muda mfupi tangu kujitokeza
hupotea baada ya muda mrefu wa matumizi ya mara kwa mara ya chakula hiki.
Ukizingatia tiba hizi pamoja na masharti ya
kufuata ukiwa unaugua ugonjwa huu yaliyoainishwa huko mwanzoni, kuna uwezekano
mkubwa wa kupona tatizo hili na kuendelea kuishi maisha yenye furaha.
No comments:
Post a Comment