Monday, February 13, 2017

MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO


Kama yalivyo magonjwa mengine, vidonda vya tumbo vina madhara endapo havitapatiwa tiba ya uhakika au endapo mhusika atashindwa kufuata maelekezo aliyopewa na daktari kwa ukamilifu wake.  Miongoni mwa madhara yake ni kama yafuatayo:

a)      Wakati mwingine husababisha kufanyika kwa upasuaji mkubwa tumboni ili kuondoa eneo lote lililoathirika endapo tatizo halikupatiwa ufumbuzi mapema.

b)      Kupungua kwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa na hali hii mara nyingi huwakuta wanaume.

c)       Uwezo wa kufanya kazi kwa ufasaha hupungua.

d)      Kulika kwa utumbo hali inayoweza kupelekea kuvuja damu kwa ndani.

e)      Msongo wa mawazo.


f)       Kifo

Soma pia JINSI YA KUBAINI VIDONDA VYA TUMBO
Share:

1 comment: