Tiba ya tatizo la msukumo mdogo wa damu hutegemeana na
chanzo chake hususani kama tatizo limekuwa sugu. Msukumo mdogo wa damu ambao unatokana na
mzio, maambukizi au mshtuko huhitaji tiba makini zaidi. Lakini zifuatazo ni baadhi ya vidokezo muhimu
vinavyoweza kusaidia katika kulitibu tatizo hili:
·
Usisimame eneo moja kwa muda mrefu
·
Epuka mazingira kame na yenye joto
·
Kula chakula kiasi lakini kilichokamilika
Ikiwa bado tatizo la shinikizo dogo la damu linazidi
kukusumbua jaribu kuonana na daktari kwenye kituo cha afya na kumpa historia ya
mabadiliko yako kiafya bila kificho chochote.
·
Kunywa maji mengi kwa siku. Wastani wa glasi sita mpaka nane kwa siku.
·
Fanya mazoezi ya kukimbia au kutembea kwa mguu
ili kuruhusu mzunguko wa damu mwilini kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.
·
Tumia viungo kama binzari, tangawizi, pilipili
ili kuongeza msukumo wa damu mwilini.
·
Tumia chumvi ya kutosha ili kurejesha kiwango
cha electrolytes ambacho kimepotea mwilini.
·
Tumia juisi ya limao iliyowekwa sukari kiasi.
·
Shiriki baadhi ya michezo kama YOGA kwani
husaidia kufanya mzunguko wa damu uwe katika hali nzuri.
Aina ya Vyakula Unavyopaswa
Kula
Ufuatao ni utaratibu wa vyakula ambavyo vinapaswa kutumiwa
na mgonjwa wa shinikizo dogo la damu ili kuweza kupambana na tatizo hilo.
Punguza kula vyakula vya wanga kama viazi, wali na mkate.
·
Kahawa inatajwa kuongeza msukumo wa damu mwilini
lakini ni vema ukapata ushauri wa daktari kabla ya kuitumia kutokana na yenyewe
kuwa kisababishi cha matatizo mengine ya kiafya.
·
Tumia vyakula vyenye asili ya chumvi ili
kuboresha mzunguko wa damu mwilini.
·
Kunywa kiasi kikubwa cha maji kwa siku kuanzia
glasi sita mpaka nane.
·
Kula vyakula vyenye protini na vitamin B
complex, na Vitamin C vikiwemo mayai, maziwam nyama n.k
Tanx a lot..nasumbuliwa sana na hili tatizo
ReplyDeletekaka umepona?
Delete