Tikitimaji ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa wingi
nchini likiwa na virutubisho vingi vyenye faida kubwa ndani ya mwili wa
mwanadamu.
Tunda hili ni chanzo cha protini, mafuta, nyuzinyuzi, wanga,
calcium, phosphorus, potassium,
magnesium, carotene, chuma, Vitamini A, B6 na C.
Licha ya kupatikana kwa bei nafuu, tunda hili huuzwa sehemu
tofauti. Kwenye baadhi ya maeneo hata
vipande vyake vinapatikana. Ingawa haishauriwi
kula matunda yaliyomenywa, vipande vya tikitimaji huuzwa barabarani pia.
Hata hivyo, tikitimaji lina faida nyingi mwilini
zinazotokana na wingi wa maji iliyonayo.
Wataalamu wanaeleza kwamba asilimia 92 ya tunda hilo ni maji. Ni muhimu kwa afya na meno na fizi.
Linakinga uharibifu wa seli huku likisaidia uyeyushaji wa
protini kuwa nishati na hurahisisha mzunguko wa damu mwilini.
Vilevile huondoa sumu mwilini na kwa mwanaume anayekula
mbegu zake husaidia kuongeza nguvu za kiume.
Huimarisha kinga za mwili na kuharakisha kupona kwa vidonda na majeraha.
Tikitimaji lina kiwango kikubwa cha Iycopene kuliko matunda
au mboga zozote za majani.
Wengi hula tunda bila kufahamu faida lukuki ilizonazo. Iwe kwenye sherehe au hotelini na wakati
mwingine nyumbani, tikitimaji ni rafiki wa afya.
Wengi wanaokula tunda hili hutema mbegu zake lakini
zikitafunwa na kumezwa faida zake ni nyingi kwa afya ya mlaji.
Wataalamu wa masuala ya lishe wanasema mbegu za tikitimaji
zina protini nyingi hivyo kuzitafuna kunaweza kumpatia mlaji chanzo cha
virutubisho hivyo. Pia, ladha yake
wanailinganisha na mbegu za alizeti.
Vilevile, mafuta yaliyopo kwenye mbegu hizo
hayana lehemu kwa kiwango kikubwa hivyo kutosababisha kuziba kwa mishipa ya
damu hivyo kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kiharusi. Zipo mbegu nyingi za tikitimaji, ni nzuri kwa
mwili wa mwanadamu.
No comments:
Post a Comment